Naibu Waziri wa Kilimo fukuza viongozi wa MAMCU- Masasi

KING DUBU

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
919
1,239
Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili sasa Korosho za wakulima zimeshindwa kwenda mnadani katika vyama vya msingi vilivyo vingi kama si vyote.

Kinachoelezwa chanzo ni ukosefu wa Magunia ya kuhifadhia na kusafirishia Korosho. Hali hii inaharibu kama si kuua soko la Korosho ambalo linaingiza mapato makubwa hapa Tanzania.

Wananchi walio wengi mbumbumbu wanalalamika bila msaada wowote huku viongozi wa kisiasa nao wakionekana hawana msaada kwao.

Hivyo waziri wa kilimo shughulikia tatizo hili ili Korosho ziende sokoni na wakulima wapate sitahiki zao japo bei yenyewe ni chini ya 2500.

Ni vipi magunia yakosekane wakati wakulima wanakatwa zaidi ya Tsh 261 ambayo ndani yake fedha ya kununulia hayo magunia IPO?
 
Mbona kipindi Cha Mwamba hamkuja na nyuzi za kuhamasisha wakulima kuandamana kudai pesa zao halali?

Alafu acha kuchongea watu mkuu ili wapoteze ugali wao.
 
MAMCU tatizo la magunia limekuwa sugu, alafu mbaya hata kupeleka korosho zao kwenye wilaya jirani zenye magunia wanakatazwa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom