Naibu waziri wa habari: "Vyama vinavyoshiriki premier ligue vianzishe viwanja vyao"

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Naibu waziri wa habari na michezo leo kanitolea mpya pale aliposema "Vyama vinavyoshiriki premier ligue vianzishe viwanja vyao vya mpira" akitolea mfano timu za Mtibwa, Azam na Yanga. Halafu pale kwenye madaraja ya viwanja mi sikuelewa kabisa. Kuna viwanja vikubwa kama Ccm Kirumba kaupa daraja la tatu wakati Chamazi kauweka katika kundi la viwanja vya daraja la kwanza pamoja na Uwanja wa Taifa na Uhuru. Hawa mawaziri wa JK hawa!
 
kosa lake ni nini, tueleze ili nasi tuelewe.

kwanza hatuiti vyama tunaita timu/club.Pili hajafafanua madaraja yamekaa vyp na tatu amekuwa akitoa maneno ya utata sana hasa kwenye mpira wa miguu kitu ambacho kinadhihirisha haijui vizuri kazi yake.
 
Amenena vyama kabisa haiwezekani klabu kongwe kama simba zinakuwa hazina uwanja!! timu zina vitega uchumi vingi, rasilimali nyingi na idadi lukuki ya wanachama, washabiki na wanazi kwa nini zisijenge viwanja vyao?? Timu iliyokamili inatakiwa kuwa na uwanja wa mechi na uwanja wa mazoezi, AZAM FC mfano wa kuigwa!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom