Naibu Waziri wa Fedha hakuweza kuongea kama Mtaalamu wa Fedha mpaka Waziri wa Katiba anakuja kuongea kwa niaba ya Waziri wa Fedha

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,781
7,541
Nimemsikiliza Naibu Waziri wa Fedha Bungeni mwana mama kwa kweli nimeshtuka sana, kwanza hakuweza kuongea kama mtaalamu wa fedha hotuba yote anasoma mbaya zaidi anasoma kama mtoto aliye darasani akijifunza kusoma.

Kuna faida kama naibu unashindwa kukaimu waziri ambaye hayuko bungeni mpaka Waziri wa Katiba ndio anakuja kuongea kwa niaba ya waziri wa fedha. Huyu mama kwa kweli hafit na hafai sasa baada kumsikia kwenye kusoma ni kama kaandikiwa anasoma bila kujuwa anasoma nini.
 
Huyu Mama hata kwny kuapa kiapo cha Unaibu Waziri ilikuwa Mushkeli kweli

Sijaelewa Dr Ashatu, Naibu Waziri wa Fedha 2015~2020 sijui kamtibua jambo gani Mzee hadi kamtema, maana kwanza ni Mwana Mama, pili ni msomi wa kiwango cha PhD , tatu aliwahi kuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe na alionekana kwa Mtazamo wa nje ni Mwenye uwezo mzuri tu

Hata kama ku balance mambo ya Muungano ndio sababu unaibu akapewa M Znz basi bado kuna wa Znz wengi tu wenye uwezo

Mamlaka za Vetting zinazomsaidia Rais sijui kama na zenyewe zilihakikiwa kabla ya kupewa nafasi hizo
 
Mm mwenywe japo sijasoma ila yule mmama hajielewi hata kidogo anajibu maswali kwa uoga uoga utazani anaoga nje!

Ila ndio wasomi wa kiafrica vichwa vimejaa majivu
 
Huyu mama ule uweupe wake na uzuri wake nafikiri vimechangia kumuweka pale atakuwa ni chakula cha mtu Fulani tu, kwanza hata kwenye kuapa nilishangaa sana yeye kuapa zaidi ya Mara tano huku akijichekesha mbele ya Rais na kuachwa huku yule mbunge wa kilwa kakosea Mara mbili tu akaambiwa kapumzike hauwezi uwaziri
 
Kazi zinafanywa na mtu mmoja ndiyo maana analalamika sana, ni mateso au naongopa ndugu zangu
 
Ukiwa kiongozi ukafanya kazi zote mwenyewe jua umeshindwa kuchagua watu wenye uwezo wa kukusaidia.
 
Huyu mama ule uweupe wake na uzuri wake nafikiri vimechangia kumuweka pale atakuwa ni chakula cha mtu Fulani tu, kwanza hata kwenye kuapa nilishangaa sana yeye kuapa zaidi ya Mara tano huku akijichekesha mbele ya Rais na kuachwa huku yule mbunge wa kilwa kakosea Mara mbili tu akaambiwa kapumzike hauwezi uwaziri
Wanaume tuna taabu
 
Mimi nadhani Mwigulu ndiye alistahili kuwa naibu Waziri wa Fedha. Angeondolewa kule kwenye uwaziri wa Katiba apelekwe kuwa naibu Waziri wa Fedha.

Huwa nikimsikiliza Mwigulu akiongelea mambo ya Sheria na Katiba huwa hana tofauti na huyo mama naibu.
 
Sijaelewa kuwa alishindwa kusoma hutuba ya bajeti au ni kujibu tu maswali???Nijuavyo ni kuwa kama waziri hayupo basi naibu wake hawezi kusoma bajeti hadi waziri mwingine kamili ndio aisome...Kama mwigulu alisoma bajeti naona ni sawa
 
Back
Top Bottom