Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,059
Alikuwa kwenye kipindi cha kikaangoni EATV amefunguka mambo kadhaa likiwemo mshahara wake ambao amesema ni milioni 3.4 na gari ya Land Cruiser ya milioni 130.
Ajira za walimu kuwa zitatoka baada ya uhakiki kumalizika.
Wanafunzi wanaotaka kusoma masomo ya Arts wasome tu ila kama wanaweza kusoma sayansi ni bora zaidi kwa kuwa ndio kipaumbele.
Pia amesema Diploma ni kigezo cha kujiunga chuo kikuu kama diploma hiyo inatambulika rasmi na taasisi zinazopima mafunzo ngazi mbalimbali.
Amelinganisha elimu ya sasa na ya miaka kumi na kusema ni bora zaidi kwa kuwa ya zamani kulikuwa hakuna walimu na nyenzo nyingine za elimu.