Naibu Waziri wa Elimu akanusha wanafunzi kubaguliwa kwa kufuata vyama vyao vya Siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Waziri wa Elimu akanusha wanafunzi kubaguliwa kwa kufuata vyama vyao vya Siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SG8, Jul 4, 2011.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,205
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 180
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo amekanusha kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma hawabaguliwi kufuatana na itikadi zao za vyama. Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu kunyanyaswa kwa wanafunzi waliofukuzwa kwa sababu ya mgomo uliojitokeza takribani wiki mbili zilizopita. Awali swali hili liliulizwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema) John Mnyika lakini Naibu waziri ama kwa kukusudia au kwa bahati mbaya hakulijibu. Itakumbukwa kuwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya wakiwa katika ziara UDOM walishauri wanafunzi wanachama wa CCM tu ndio walirudishwe Chuoni huku wale wa Chadema wakiachwa nyumbani kana kwamna watanzania na wanafunzi wote wa UDOM wameganyika katika vyama hivyo viwili tu vya siasa
   
 2. N

  Nzogupata Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anakanusha nini kilaza mulugo? ajiulize nae kuwa kama angekuwa na mtoto ama ndugu ktk kundi hilo la waliobaki na akasikia wakuu wa wilaya wameenda udom nakuomba wale wanachuo wenye itikadi ya ccm tu ndo warudi na mwanae akawa miongoni mwa ambao hawajarudi, angejisikiaje?Lakini pia mbona baraza la mawaziri na serikali kwa ujumla imeelemewa na huu ugonjwa wa mdai haki nchini kuwa na cdm tu? Kwa maana nyingine serikali inapenda vilaza kwa maana wale wa ccm ambao hawana tabia yakuhoji hata kama wanaona mambo hayaendi vizuri.Mi nadhani ukiend ndani sana utakuta hata itikadi ile ingine imezingatiwa
   
 3. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu kazi kweli kweli!nchi yetu hii inahitaji kuadabishwa 2015!
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,703
  Trophy Points: 280
  Fafanua.........
   
Loading...