Naibu Waziri wa Ardhi azitaka Halmashauri nchini kupanga Miji kuepuka migogoro

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka Halmashauri nchini kuhakikisha zinapanga, kupima na kumilikisha ardhi ili kuepuka migogoro ya ardhi pamoja na kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi.

Dkt Mabula alitoa agizo hilo jana mkoani Kigoma wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi wa halmashauri nane za mkoa huo akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi. Halmashauri hizo ni Buhigwe, Kasulu DC, Kasulu TC, Kakonko, Kibondo, Kigoma DC, Kigoma MC, na Uvinza DC.

Alisema, wakurugenzi wa halmashauri wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu la kusimsmia halmashauri zao ili ziwe na miji yenye mpangilio mzuri ambapo alibainisha kuwa kama maeneo ya miji hiyo yataachwa bila kupangwa, kupimwa na kumilikishwa basi yatakuwa hovyo na maeneo mengi kuingia kwenye zoezi la urasimishaji.

‘’ Halmashauri zote nchini jukumu la kupanga miji ni la kwenu Wizara itasimamia nidhamu na ajira na mkizubaa katika hili miji itaendelea kuwa mibaya na serikali haitaki kuona ujenzi holela ukiendelea’’ alisema Naibu Waziri Mabula.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, urasimishaji unaofanyika sasa katika maeneo mbalimbali umesababishwa na kasi ndogo ya upangaji miji unaofanywa na halmashauri na kinachofanyika katika zoezi hilo ni huruma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi na kubainisha kuwa mwisho wa zoezi la urasimishaji ni mwaka 2023.

Alisema, hata idadi ndogo ya hati zilizotolewa katika halmashauri za mkoa wa Kigoma ni ishara ya kasi ndogo ya upangaji na upimaji katika mkoa wa Kigoma ambapo Naibu Waziri Mabula alishangazwa na halmashauri za Kigoma DC na Kasulu DC kwa kushindwa kutoa hata hati moja katika kipindi cha nusu mwaka huku halmashauri ya Buhigwe ikitoa hati sita tu na hivyo kuutaka mkoa kuhakikisha unazisimamia halmashauri hizo ili ziweze kupanga, kupima na kumilikisha maeneo mengi zaidi.

Kuhusu suala la mapato ya kodi yataokanayo na ardhi, Naibu Waziri Mabula ameoneshwa kutofurahishwa na kasi ya ukusanyaji mapato katika mkoa wa Kigoma ambapo kwa kipindi cha nusu mwaka 2019/2020 halmashauri za mkoa huo zimekusanya shilingi milioni 312,233,500.9 sawa na asilimia 13 tu huku Kigoma DC na Kasulu DC zikiwa zimekusanya mapato ya ardhi chini ya asilimia 1.2 na halmashauri pekee iliyofanya vizuri ni Kakonko iliyokusanya milioni 17,281,142.59 sawa na aslimia 28.

‘’Kama taasisi nyingine za serikali kama TRA zingekuwa hazikusanyi kodi kama ulivyo mkoa wa Kigoma katika suala la ardhi ambapo mna asilimia 13 tu basi miradi mikubwa inayofanywa kwa kutumia kodi za ndani ingekwama’’ alisema Dkt Mabula.

Awali Afisa Ardhi wa mkoa wa Kigoma Jairo Pilla katika taarifa yake ya nusu mwaka 2019/2020 ya utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Kigoma alisema, kiwango kidogo cha kodi ya ardhi kilichokusanywa kwenye mkoa wake kimesababishwa na sehemu kubwa ya ardhi kwenye mkoa huo kutopimwa na kumilikishwa.

Aidha, alisema suala lingine lilichongia mapato kidogo ya ardhi ni idara ya ardhi kutopewa kipaumbele na halmashauri za mkoa huo ambapo hakuna bajeti inayotengwa kwa ajili ya kupanga na kupima maeneo na kitu pekee kinachofanyika ni zoezi la urasimishaji na kusisitiza michoro mingi inayowasilishwa ni ya urasimishaji tu.
 
Miji anaweza panga Mzungu, toka lini MTU mweusi akaweza mipango miji, Dar es salaam si hii hapo, mji nao huo au mrundikano wa watu? Urban planning ni reflection ya uwezo wa kufikili, angalia watu walivyojipanga kwenye majabari ya milima Mwanza, serikali ilikuwa wapi? Nenda kwenye milima ya nchi za wenzetu, miji kama London, New York imepangwa more than 200 years ago, sisi tumeweza lipi?
 
Hii nchi ya ajabu sana, Chuo kikuu cha Ardhi kila mwaka kinatoa wataalamu wa Mipango Miji tokea 2016 hakuna wanaoajiriwa na serikali kuu wala SM na wakati wao ni sehemu ya utatuzi mkubwa wa kazi ya kupanga na kugawa mipango miji ingeenda kwa kasi lakini wamekaa na kusubiri Rais atasema lini.

Sasa hivi vijana wako tuu mitaani maana hawana pengine pa kwenda kuajiriwa kwani fani hiyo mwajiri ni serikali tuu na yenyewe imepigwa bumbuazi na hata waziri naye analalamika
 
Hivi naibu Waziri ana ushawishi gani kwenye awamu ya 5 ambayo hata kuzindua stendi ya daladala tu ni lazima aende Rais ? Mwambie huyo jimbo alilopewa huko Mwanza lilishamshinda uchaguzi ujao atafute kazi , tutamng'oa bila huruma yoyote .
 
Ushaona city gani duniani linalo deserve kuitwa city likakosa Parks? Kama unataka kujua tofauti ya akili ya MTU mweusi na Mzungu nenda Pretoria SA kaangalia ule mji ulivyopangwa, ndio utajua kwann ma Prof wetu wanasema wameokotwa majalalani, na wala hakukosea kusema hivyo!!
 
Mimi kina wakati huwa nashindwa kushangaa
Mfano labda mimi nataka kufuga ng'ombe wa ndani 'zero grazing'
Sijajua ni aina gani ya kiwanja naweza pata. Maana mipangomiji wao ni makazi na fremu na maeneo ya wazi na michezo. Kiukweli ilitakiwa yawepo maeneo hata ya ufugaji wa zero grazing au kuku au hata mbuzi.
Anyway Mipango miji changamoto ni nyingi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom