Naibu Waziri wa Afya, Ndugulile: Upimaji wa UKIMWI kuhamia viwanja vya michezo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile amesema wana mpango wa kuhamishia kambi ya upimaji virusi vya ukimwi kwenye viwanja vya michezo ili kuhamasisha wanaume kujitokeza kupima.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya kutembelea maonesho ya Utamaduni ya Jamafest, Dk Ndungulile alisema sababu kubwa ya kutaka kuhamishia kambi viwanjani ni baada ya kugundua wanaume wengi wanakwepa kupima, huku baadhi yao wakionekana kufa zaidi kwa kutozingatia maelekezo.

“Wanawake wengi wamekuwa wakijitokeza kuliko wanaume, tumeona twende kwenye makambi kuwafuata na mojawapo ni viwanja vya michezo ili kutoa elimu ya upimaji kwao,”alisema.

Alisema hata kwa baadhi wanaokutwa na maambukizi huchelewa kuanza dawa za kuua makali jambo ambalo limechangia baadhi kufa mapema huku akiwahimiza kuuona ugonjwa huo wa kawaida kama yalivyo mengine.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo alisema ujio wake katika tamasha hilo una mahusiano makubwa na Utamaduni kwasababu wamekuwa wakifanya kazi n’a wasanii mbalimbali kufikisha jumbe za afya.

“Michezo, sanaa na Utamaduni yana mahusiano tumekuwa tukifanya nao kazi, lakini pia ningependa kuona wasanii wanaibua mada mbalimbali za afya kwa mfano masuala ya lishe na mambo mengine tuweze kuyafanyia kazi,”alisema.

Alizungumzia Jamafest alisema ameona kazi nyingine nzuri na kuona kuna bidhaa nyingi ambazo zinauzwa kuuzwa nje na kuwapongeza wizara ya Habari na Maliasili na utalii kwa maandalizi mazuri.

Alisema tamasha lijalo wawashirikishe wawe pamoja kwani kuna mambo mengi yanahitaji kuzungumziwa kwa ushirikiano na wasanii.
 
Tunaomba wasanii wa bongo movie na bongo flavour wawe wanahudhuria uwanjani kama wahamasishaji........ 97% wanao.
 
Back
Top Bottom