Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile aelezea aina za Barakoa za kuvaa na Utaratibu wa kutengeneza ya kitambaa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
72,865
2,000
Kuna haja kubwa sana kwa Masuala ya Afya kuzungumzwa na wataalam wa Sekta hiyo tu na si vinginevyo , mtu aliyesomea Kahawa na vitunguu hawezi kuyajua mambo haya .

======

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile, ametolea Ufafanuzi Clip inayosambazwa.

Naibu Waziri amesema:
1587307295159.png

=> Kuna clip inazunguka nikiongelea kuhusu barakoa za kitambaa. Napenda kutoa ufafanuzi ufuatavyo:

=> 1. Barakoa za N95 zinapaswa kutumika na watoa huduma wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Covid-19. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa mitaani, majumbani wala maofisini."

=> "2. Barakoa za upasuaji (surgical masks) hizi zinapaswa kuvaliwa na watumishi wa afya ambao hawana direct contact na wagonjwa. Barakoa hizi pia zinaweza kuvaliwa na jamii kwenye maeneo ya mikusanyiko kwa muda wa masaa 4-6."

=> "Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa kutwa nzima na kurudia matumizi (re-use). Aidha, kumekuwa na sintofahamu kuhusu namna ya uvaaji wa barakoa za upasuaji."

=> "Barakoa hizi zinapaswa kuvaliwa kama ifuatavyo:

(a). Upande wenye rangi (blue, kijani, zambarau nk) unapaswa kuwa nje.

(b). Upande wenye chuma unapaswa kuwa juu."

=> "3. Barakoa za kitambaa (cloth masks) hazina ubora wa kinga kama N-95 au surgical masks, lakini zinaweza kutumika kupunguza uwezekano wa maambukizi toka kwa mtu mmoja kwenda mwingine majumbani na sehemu za mikusanyiko."

=> "Mambo ya kuzingatia ni pamoja na kutumia vitambaa vya pamba, kutumia layers zaidi ya mbili katika utengenezaji wa barakoa hizo, kuwa na barakoa angalau mbili ili kuruhusu kufanyiwa usafi wa mara kwa mara na barakoa zifuliwe kwa maji na sabuni na kupigwa pasi."

=> "Ni muhimu kukumbuka kuwa barakoa sio mbadala wa kunawa mikono na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu (Social distancing) bali ni nyongeza ya hatua hizi."

=> "Tuhakikishe barakoa zilizotumika hazitupwi ovyo na badala yale zichomwe moto ili kuepuka kuokotwa na kutumiwa na watu wengine. Vile vile, watu hawapaswi kuazimana barakoa iliyokwisha kutumika. Kila mtu awe na yake."

=> "Mwisho, tuendelee kuzingatia maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Wizara ya Afya kuhusu hatua mbali mbali za kujikinga na ugonjwa huu."
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
2,470
2,000
Mbona mnatuchanganya sana! hivi Serikali hii ni yupi ambae tunapashwa tumsikilize? Na yupi ambae ni msemaji wa Serikali juu ya maswala ya kitalamu kuhusu Corona?

Je Makonda kwenye mkoa anao uongoza hana watalamu na wenye akili za kushindwa kuwatumia Katika kipindi hiki kigumu,ukiacha na Waziri je RMO wa Dsm anakazi gani? Au Makonda anakaimu nafasi ya RMO.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
1,135
2,000
Mbona mnatuchanganya sana! hivi Serikali hii ni yupi ambae tunapashwa tumsikilize? Na yupi ambae ni msemaji wa Serikali juu ya maswala ya kitalamu kuhusu Corona? Je Makonda kwenye mkoa anao uongoza hana watalamu na wenye akili za kushindwa kuwatumia Katika kipindi hiki kigumu,ukiacha na Waziri je RMO wa Dsm anakazi gani? Au Makonda anakaimu nafasi ya RMO.
Ujue tatizo ni kwamba, hata hao tunaopaswa tuwasikilize sio wataalamu wa Afya, ni full kuchanganyana tu.

Tuliambiwa tumsikilize Rais, M/Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, na mwingine mmoja, niambie, kati ya hao nani mwenye utaalamu wa hayo mambo?

Utakuta wanapewa ushauri mzuri na wataalamu wa Afya, then badala waulete kwetu kama ulivyo, wanauchanganya na ujuaji wao kidogo, matokeo yake ukifika kwetu unakuwa haueleweki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Careem

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
20,721
2,000
Watanzania hatuzidi milioni 60 kwanini basi serikali isitoe tu Milioni 60 ili kila mtanzania apewe milioni 1 imsaidie katika kipindi hiki cha Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio umetoa wazo zuri sana.

"Cᵒᵃᶜᵏʳᵒᵃᶜʰ ⁿᵘʰ ᵇᵘˢˢⁱⁿᵉˢˢ ⁱⁿⁿᵃ ᶠᵒʷˡ ᶠⁱᵍʰT"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom