Wizara ya Afya Tanzania
Official Account
- Oct 1, 2020
- 58
- 124
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amebaini wizi wa dawa unaofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa ambapo katika ushahidi alionao amesema kuwa Idara ya Famisia imehusika katika upotevu wa dawa za thamani ya Tsh Milioni 9.
Dkt. Mollel amesema hayo katika kikao kazi na watumishi wa hospitali hiyo ambapo alimwita Mfamasia wa Hospitali hiyo pamoja na Mganga Mfawidhi kuhakiki taarifa hizo alizonazo na wote kukiri kuwa ni kweli.