kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Nimemsikiliza Naibu Waziri wa Afya akiwa Longido, Kwanza haeleweki ameenda kukagua nini. Haeleweki anavyozungumzia mapungufu katika ujenzi wa kituo cha afya tatizo ni mganga mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Mkandarasi au ni kiumbe gani anapaswa kulaumiwa na kwa makosa gani.
Pamoja ukweli kwamba hata wanaomsikiliza hawamuelewi, ameenda mbali zaidi na kumsimamisha kazi Mganga Mkuu, sijui mganga mkuu ndiye anayekusanya fedha za ujenzi wa hospital kwa wananchi?
Haya mamlaka Mganga wa Wilaya anayatoa wapi? Mkurugenzi kazi yake nini? Je mkuu wa Wilaya wa eneo ilo alikuwa wapi asione tatizo hadi naibu wa Waziri aliyetumia chini ya masaa mawili aone tatizo, alifanyie uchunguzi na kutoa hukumu?
Kwa aina hii ya Mawaziri nadhani itatuchukua dahari na dahari kuendelea. Tuheshimu taaluma za watu na tutendee haki taaluma zetu.