Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel atoa ufafanuzi kuhusu "Matatizo ya Kushindwa Kupumua"

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,930
2,000
Kama hujaelewa hapa basi utakuwa na Chuki binafsi

======

Akihojiwa na Mwananchi, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ameeleza haya:

Kwanza hamna taharuki kubwa kwa huu mwaka kama ilivyokuwa mwaka 2020. Mwaka wa 2020 tatizo hilo lilivyotekea taharuki haikuingia tu Tanzania, ilikuwa dunia nzima na sisi Tanzania ni sehemu ya dunia.

Lakini kwa kutumia sayansi na ushauri wa wanasayansi, Rais wetu alikuja na muelekeo ambao muelekeo huo ndio uliotunusuru sisi leo hapa Tanzania.

Alitoa muelekeo ambao unasema tutafuata taratibu zote ambazo zinatakiwa za Shirika la Afya Duniani; tutafuata ushauri wa wanasayansi wa nje na wetu. Lakini tutatumia namna ambayo inaangalia hali yetu.

Unajua unapo-deal na masuala ya afya, ni lazima utumie cultural sensitive approach. Tutaangalia mila na desturi za eneo husika, tutaangalia hali ya uchumi wa eneo husika, kabla ya kuja na strategy yoyote.

Na usipofanya hivyo maana yake ni nini? Unapoanza kutafakari kwa kufikiria ugonjwa mmoja tu, kwa maana tungekubaliana na watu wanavyotaka, tuka-narro mind zetu ku-deal na Corona pekee...Kipindupindu kingepanda, TB ingepanda na magonjwa mengine yangeendelea kuwaua watu.

Sisi Tanzania tunapsema Matatizo ya Kupumua, hata ukienda WHO oukiangalia kwenye data zao utaona wakati mwingine wana-categorize magonjwa duniani yanayoongoza kwa kuua, utaona kuwa magonjwa yanayotokana na maambukizi ya kupumua yamewekewa kwenye bracket mambo mengi yanayoweza kuayasababisha.

Approach iliyochukuliwa na Tanzania mwaka 2020 ni approach ambayo inatumiwa na dunia nzima, na watu wengi hawapendi kusema hilo.

Sasa hivi tumeamua ku-categorize haya ni magonjwa ya kupumua lakini nenda kwenye taasisi yetu ya moyo na zungumza na madaktari wa moyo. Mgonjwa anapofika kwenye emergency department moja ya dalili anazokuwa nazo ni kushindwa kupumua. Nenda kwa watu wetu wa matatizo ya sukari, anapokuja mgonjwa kwenye emergency department, moja ya presentations ni kushindwa kupumua.

Uliza watu wa emergency medicine, anapokuja mgonjwa wa pneumonia au pumu, moja ya dalili zake ni kushindwa kupumua.

Mwaka 2020 kilichotutokea, watu walisema Corona! Corona! Corona! Matokeo yake kila anayekuja ana joto na anashindwa kupumua anaitwa Corona, kumbe huyu mtu ana presha; kumbe huyu mtu ana sukari.


 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,930
2,000
Kwahiyo hilo tatizo la sukari na pressure kusababisha watu kushindwa kupumua limeanzia kwenye awamu hii ya tano? Mana awamu za nyuma kabla ya corona hatukuwahi kusikia tatizo kama hilo
Kijana acha kubishana na wakubwa
 

mzushi

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
3,042
2,000
Huyu mwenda wazimu tu kama walivyo wendawazimu wengine, tofauti yao huyu anaficha uendawazimu wake kwa kuvaa suti wenzake wanatembea uchi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom