Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.

Dk Mollel pia ameagiza Koroso aswekwe mahabusu akidai amemtolea majibu na lugha ya kijeuri kuwa “hajali lolote hata akifukuzwa kazi”.

Dk Mollel ametoa maagizo hayo Julai 5 akiwa mjini Nansio Ukerewe alipofika kutatua mgogoro uliobuka kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya mkoa katika kisiwa hicho ndani ya Ziwa Victoria.

"Kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye mradi huu, Koroso utakoma kuwa mkuu wa Idara ya Ujenzi Wizara ya Afya. Katibu mkuu atamteua mkuu mpya wa idara ambaye atakuja kusimamia mradi wa Ukerewe," alitangaza Dk Mollel.

Pamoja na viongozi na wataalamu wa Wizara, mkoa na wilaya, kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa CCM, halmashauri na mkandarasi Suma JKT.

Miongozi mwa malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe dhidi ya Koroso ni kutowashirikisha viongozi wa wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa mradi huo.

"Ofisi ya DC, halmashauri na CCM Wilaya ya Ukerewe hawakushikishwa katika utekelezaji wa mradi huu," Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila alimweleza Dk Mollel.

Muda mfupi kabla ya amri ya kuswekwa mahabusu, Koroso alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Serikali ingeokoa kati ya Sh180 milioni hadi Sh260 milioni iwapo ungetekeleza mradi huo kwa mtindo wa Force account (kutumia nguvu za wananchi) badala ya ukandarasi.

Kiwango kilichotajwa na Koroso kilitofautiana na kiwango cha Sh600 milioni kilichotajwa na mhandisi wa mkoa wa Mwanza, Chagu Nghoma.

Kutokana na tofauti hiyo, Dk Mollel akamtaka Koroso kutoa ufafanuzi, ndipo akasisitiza kuwa hesabu zake ndizo sahihi kwa mujibu wa kanuni na msingi wa kitaaluma na kwamba yuko tayari kuchukullwa hatua yoyote.

"Mheshimiwa Naibu Waziri, kiwango nilichotaja kimezingatia kanuni, vigezo na hesabu za kitaaluma; nitaendelea kusisitiza hilo hata kama ukinifukuza kazi sitajali," alisema Koroso.

Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu.

Chanzo: Mwananchi
 
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.
Huyu jamaa sura yake ilivyokaa kaa tu anaonekana na disorder flan sijui unaibu waziri kaupataje
 
Tangu lini Naibu Waziri amekuwa na mamlaka ya kumtia mtu ndani? Au hata kumshusha cheo mtumishi wa umma? Tangu lini kumjibu vibaya kiongozi yeyote imekuwa kosa la jinai?

Hivi nani atamfungulia mashtaka huyo Injinia? Na hao ma dc na wengine wametajwa wapi katika mkataba? Kushirikishwa kwao ni privilege sio right. Wao kama wanataka iwe right, waiingize kwenye mkataba wa ujenzi kuwa msimamizi wa mradi atawajibika kwa DC na kamati zake.

Alipokosea injinia ni kwenye suala la Force Account. Yeye angeishia kusema tu kuwa Suma kazi imewashinda na atafutwe mkandarasi mwingine. Force account itumike kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo na kuziba mashimo ya barabarani lakini sio kwenye miradi complex kama hospitali. Kwa kusema hivyo, nimeingia shaka na uwezo wake na huyo mwenzake wa mkoani.

Ila kwenye hili, amfungulie mashtaka Naibu Waziri kwa matumizi mabaya ya nafasi yake na kumuonea. Labda ndio yeye na wenzake watajifunza kuwa wao ni viongozi sio wanyapara.

Amandla....
 
"Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu. "

🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
Jamaa alijifanya mbabe bila kutambua kuwa ameketi sehemu na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya matokeo anawekwa chini ya ulinzi!
 
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.
Huyu jamaa sura yake ilivyokaa kaa tu anaonekana na disorder flan sijui unaibu waziri kaupataje
 
"Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu. "

🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
Jamaa alijifanya mbabe bila kutambua kuwa ameketi sehemu na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya matokeo anawekwa chini ya ulinzi!
Kuna ubabe gani kwenye majibu? Huyu naibu waziri kilaza anaamrisha mtu awekwe ndani kwa kosa gani? Jaribu kutumia akili hata kidogo.
 
Ndio maana tunahitaji katiba mpya, my minister kama uliona kuna tatizo lenye harmful ya ufisadi ilitakiwa uende kituo cha police na kumfungulia docket huyu inginia sio kutumia udikiteta uchwara kama ulivyofanya, hii ni wrong maana wote tupo chini ya sheria.
 
Ndio maana tunahitaji katiba mpya,my minister kama uliona kuna tatizo lenye harmful ya ufisadi ilitakiwa uende kituo cha police na kumfungulia docket huyu inginia sio kutumia udikiteta uchwara kama ulivyofanya, hii ni wrong maana wote tupo chini ya sheria
Naumga mkono
 
Back
Top Bottom