Naibu Waziri wa Afya aagiza safu ya uongozi wa Mount Meru kuondolewa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ameagiza kuondolewa kwa safi ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru inayoongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Shafii Msechu ikiwa ni sehemu ya maboresho katika afya.

Dkt. Mollel ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara katika Hospitali hiyo na kuzungumza na timu ya uendeshaji wa huduma za Afya ya Mkoa ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe katika ofisi za Mganga Mkuu wa Mkoa huyo Jijini Arusha.

“Tumeona kwamba, Hospitali ya Mount Meru inahitaji mabadiliko makubwa sana yakiuongozi, kwa kushirikiana na mamlaka husika, yafanyike haraka sana, kwasababu kuna mambo ya msingi sana yanayogusa Jamii ambayo yanatakiwa kufanywa kwa ustadi wa hali ya juu” alisema Dkt. Mollel.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi sana kwenye Sekta ya Afya, katika kuboresha miundombinu na huduma za afya zinazotolewa ili kuwasaidia wananchi wa vipato vya chini kupata huduma bora na nafuu bila wasi wasi.

“Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi sana kwenye eneo la Afya, Serikali imekuwa ikileta miundombinu mingi sana kwenye eneo la Afya, fedha ambazo Serikali imezileta kwenye eneo la afya zinatakiwa matokeo hizo fedha yamguse mwananchi wa kawaida” alisema.

Alisisitiza kuwa, pale ambapo fedha zinazotolewa na Serikali kwaajili ya maboresho ya huduma za afya na miundombinu hazimgusi mwananchi wa kipato cha chini, ni lazima Serikali itafanya mabadiliko ili kuboresha Sekta hiyo kutoa huduma bora na nafuu kwa wananchi.

Na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Wedson Sichalwe amesema kuwa, Serikali imeboresha miundombinu katika Sekta ya Afya na utoaji huduma ikiwemo hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata huduma bora na nafuu.
 
[SUB]namjua dr msechu bonge moja la surgeon ila alikua pale kwa mkataba. Kuna mahali walipishana maana wote walisha fanya seliani. Dr msechu ana misimamo yake pia. Ila anafanya kazi sana[/SUB]
Msechu aliwahi kufanya kazi Seliani?
 
Safu ya Uongozi Mt Meru
Medical Officer Incharge
Nurse officer Incharge
Heads of Departments
 
Back
Top Bottom