Naibu Waziri Viwanda na Biashara S. Manyanya, atumbua mtu kwenye Mahafali

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhandisi Stella Manyanya amemtumbua Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani (FCC) huku akiwakumbusha TBS na Taasisi nyingine kujitafakari.
Naibu Waziri huyo amechukua aumuzi huo wakati wa mahafali ya Chuo cha Biashara (CBE).
e82c13f16dec994495d20d456594b15f.jpg
 
..Mkurugenzi Mkuu wa FCC ana kaimu nafasi hiyo.

..amekaimishwa na Waziri wa Biashara baada Dr.Frederick Ringo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu kumaliza muda wake wa utumishi.

..Mchakato wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu mpya bado haujakamilika.

..Hebu tuletee Video Clip tuone nini kilichoendelea.
 
..Mkurugenzi Mkuu wa FCC ana kaimu nafasi hiyo.

..amekaimishwa na Waziri wa Biashara baada Dr.Frederick Ringi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu kumaliza muda wake wa utumishi.

..Mchakato wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu mpya bado haujakamilika.
Pia sina hakika kama Naibu " wa" Waziri ana mamlaka ya kutumbua papo kwa hapo!!
 
..Mkurugenzi Mkuu wa FCC ana kaimu nafasi hiyo.

..amekaimishwa na Waziri wa Biashara baada Dr.Frederick Ringo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu kumaliza muda wake wa utumishi.

..Mchakato wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu mpya bado haujakamilika.

..Hebu tuletee Video Clip tuone nini kilichoendelea.
Sasa kumaliza muda wake ndio katumbuliwa. Mtoa mada mbona kama kazingua ss
 
Pia sina hakika kama Naibu " wa" Waziri ana mamlaka ya kutumbua papo kwa hapo!!

..Jamaa aliyekuwa anakaimu ametolewa chuo kikuu ambako alikuwa mhadhiri.

..mimi naona hilo tayari lilikuwa ni kosa. Ni afadhali waziri angeteua mmoja kati ya wakurugenzi wa idara za fcc kukaimu nafasi ya mkurugenzi mkuu.

..wamechafua cv ya jamaa wa watu bure tu.

..kuhusu mamlaka ya naibu waziri kutengua mtendaji aliyeteuliwa na waziri sina uhakika na suala hilo. Lakini kama naibu waziri kamtengua basi itabidi tu watekeleze hata kama amekosea.
 
Sasa kumaliza muda wake ndio katumbuliwa. Mtoa mada mbona kama kazingua ss

..FCC for the last two to three months imekuwa ikiongozwa na KAIMU MKURUGENZI MKUU.

..Kaimu Mkurugenzi Mkuu aliteuliwa na Waziri kuziba nafasi iliyokuwa wazi baada ya Mkurugenzi Mkuu wa FCC kustaafu.

..Mchakato wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu mpya ulitangazwa kwenye magazeti na wenye vigezo walitakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

..Kwa uelewa wangu mchakato bado haujakamilika.

..Nadhani mpaka hapo umenipata.
 
Sasa huyu anakurupuka kumtumbua mtu anaekaimu?? Weledi uko wapi?? Hopeless sana huyu Mama! Eti engineer....makota....yanguu!!!!
 
Jamani hawa viongozi wafate muongozo wa Utumishi wa Umma ....Waziri au Naibu Waziri hawana mamlaka ya kufukuza Anashauri tu na si lazima ushauri wao ufuatwe uchunguzi ndio utakaoamua!

Naona sheria za Utumishi wa umma wamezisahau....semina elekezi inahitajika kwakweli mambo hayatakiwi kuwa shagala bagala hivi...wafuate ushauri aliowapa PM unaendana na kutamka mambo kama haya..hili tatizo lilianzia awamu ya nne katika wizara za Marehemu Sita na Mwakyembe na linaota mizizi linaitaji kukemewa na mamlaka za juu....

Katibu mkuu anaruhusiwa kwa either agizo la Rais kama alivyoelekeza juzi kua watoa vibali vya kuagza sukari waondolewe na wapangiwe majukumu mengine japo niliona waziri amemsimamisha kazi DG wa Bodi ya sukari kama ndiye anayetoa kibali ni sahihi ila kama siye nazan waziri atakua alikosea na Waziri alitakiwa amwagize Katibu mkuu atekeleze agizo cz ndiye mwajiri ndani ya Wizara haya masuala yakifka kwenye mahakama au CMA mtumishi akikata rufaa atatumia hizo techinicalty kushinda kesi na atalipwa fidia kubwa ambayo si pesa ya Waziri au Naibu Waziri ni kodi za Watanzania Wizara Ya Utumishi itoe muongozo kwa wizara zote ni jukumu lao si kila kitu wamsubiri Mheshimiwa Rais..

Makamu au Waziri Mkuu hao viongozi wa juu wana majukumu mengi lazima wizara husika isaidie tunakoelekea serikali itakuja kulipa fidia zisizo na msingi masuala ya kitaalam hayaitaji siasa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom