beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, amesema kumekuwepo na tabia ya Viongozi wa timu mbalimbali Nchini kutoa kauli za kwamba walihongwa hususan wanapofungwa na Yanga.
Akiwa Bungeni Dodoma amesema, "Ifike wakati Viongozi wa Timu hizi na Watanzania kwa ujumla wakubali kwamba Yanga ndio Timu bingwa hapa Tanzania na bora Afrika, kwahiyo wanapofungwa wakubaliane na matokeo"
Aidha, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema Serikali haitofumbia macho wanaotumia Rushwa kujipatia ushindi.