Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Kumekuwepo na lawama nyingi ambazo zimekuwa zinaelekezwa kwa Serikali na wananchi, wakiwemo wabunge, kwamba Serikali ilimtelekeza na kumdhulumu haki yake ya ubunifu wa nembo ya Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Mzee Francis Kanyasu 'Ngosha'.
Kufuatia lawama hizo pamoja na swali lililoulizwa bungeni na Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Devotha Minja ikiwa kuhusiana na suala hilo hilo ; Naibu Waziri wa Naibu wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastasia Wambura ametoa majibu yafuatayo:
"Si kweli kwamba Serikali imemhujumu Mzee Francis Ngosha, Kimsingi Mhe. Spika yapo majibu mezani kama matatu hivi yanayohusiana na ubunifu wa nembo ya Taifa ambayo tunaitumia, kwa hivyo mpaka sasa bado haijajulikana nani hasa ambaye ni mbunifu wa nembo hii".
Kwa sababu mfano yupo marehemu ambaye alishatangulia mbele ya haki muda mrefu ambaye anaitwa Abdallah Farhani wa Zanzibar yeye vielelezo tayari vishakutwa katika Kumbukumbu zake jinsi alivyokuwa akibuni nembo yetu ya taifa, nembo ya Kenya pamoja na hata ya nembo ya OAU kipindi hicho alipokuwa anasoma Makerere University".
Kwahivyo yapo majina ambayo yanadaiwa kwamba yalishiriki katika kutengeneza nembo hii.
Chanzo: Dar24