Naibu Waziri: Serikali itatumia hekima kuwasaidia ambao wameshindwa kujisajili

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Tanzania imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Hayo yameelezwa Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

“Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.

Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.

Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.
 
Kwani kusajili laini kunaongeza nguvu za kiume? Wafunge Kwanza watakuwa wamenipunguzia matumizi.
 
Anawalisha watu matango pori hivi unajuaje hii line haijasajiliwa na mwenyenayo kashasajili nyingine wakati alitumia kitambulisho jina la mtu mwingine kusajili mwamzo?
 
Back
Top Bottom