Naibu waziri p.mulugo huo ni utashi tasa wa utendaji kazi.....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu waziri p.mulugo huo ni utashi tasa wa utendaji kazi.....!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EL MAGNIFICAL, Jun 10, 2012.

 1. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndg wanabodi salamu kwenu...! pia nitumie fursa hii kuwapa pole familia, cdm na wote tulioguswa na msiba wa kamanda wetu Bob Makani.
  Leo nataka kumuweka wazi ndg philip mulugo nw elimu kuwa operation anayoendelea nayo ya kufunga shule za binafsi kisa hazijakizi vigezo ni utashi tasa wa kazi pia ni kuonesha kuwa tanzania ni nchi ya kibabe na uongozi dhalimu.
  Sisemi shule ambazo hazijakizi vigezo zisifungwe la hasha ila kuonesha uwazi katika hili ni vyema angeanza na shule yake mwenyewe southen highland ambayo nayo pia haijakizi vigezo vya kuwa shule. Kwanza ipo katikati ya makazi ya watu ambapo pande zote nne kuna nyumba za watu wengine. Pili namna ilivyojengwa pia si mazingira rafiki kwa kusomea kwani majengo yake ni ya ghorofa lakini yamejengwa kwa mabanzi pia ameyapaka rangi ambapo usipokuwa makini ni ngumu kutambua. Tatu hostel zinazotumiwa na wanafunzi ni nyumba za watu binafsi kwa mfano hostel ya wanawake ipo mbali sana na shule kiasi kwamba ni hatari sana kwa wanafunzi wa kike tayali imeshaleta madhala mengi ambayo hata yeye mwenyewe anajua. Nne shule hiyo pia haina viwanja vya michezo kabisa kwani eneo lake ni finyu kabisa.
  Ndg mlugo kama kweli una uchungu na taifa hili ni vyema ungeanza na shule yako.
  Kuhusu sehemu ambazo unafika na kukuta form six ndo wamekuwa walimu sifahaamu kinachokufanya uwe mkali ni nini maana hata wewe umeshafundisha ukiwa na elimu ya form six na hata sasa elimu yako ni utata mtupu.
  Pia ukiwa kama nb elimu usipende kuwahadaa watanzania kwamba hujui njia zinazotumika kuvujisha mitihani kwani kuna kipindi ukiwa kama mkuu wa shule, shule yako ilivujisha mtihani wa kidato cha nne na shule yako ikafungiwa hivyo basi ni wazi unazijua njia zote za wizi wa mitihani na unachofanya ni mzaha tu.
  Nahitimisha kwa kusema mpaka leo cjaona umuhimu wako kama naibu waziri na umeingia kwenye siasa si kwa lengo la kizalendo ila kugeuza utumishi kama sindano.
  Nawasilisha.
   
 2. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Mpe huyo cmpend kama nini katupigia sana dada zetu
   
 3. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  huyu bwana ni janga la kitaifa basi tuu !.
   
 4. m

  mama-lokatare Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii nchi bwana kama mchezo wa kuigiza ivi anyway mwisho wa uchumia matumbo unakuja na tutaheshimiana taratibu.
   
 5. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tatizo la nchi yetu si viongozi c wananchi bado hatujaamua kweli kweli.
   
Loading...