Naibu Waziri Nditiye aagiza TCRA kukagua mabasi yote yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1578551953584.png

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhakikisha wanasimamia na kukagua mabasi yote yanayosafirisha vipeto, bahasha na vifurushi bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka hiyo na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha mara moja.

Nditiye ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 26 wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, waliokutana kutathmini na kuweka mipango mipya ya kuimarisha Shirika hilo.

Nditiye amesema licha maagizo yake ya awali, lakini bado mpaka sasa kuna mabasi ya abiria yanasafirisha vipeto bila ya kuwa na leseni na kutaka TCRA kufanya ukaguzi wa kina kuhakikisha wanayabaini mabasi hayo na kuyachukulia hatua Kali za kisheria.

"Nataka nitoe maagizo TCRA mkafanye msako licha ya maagizo niliyotoa lakini bado Kuna mabasi bado yanasafirisha vipeto, bahasha na vifurushi wakafanye msako kuhakikisha mabasi yote yanayosafirisha yanakuwa na leseni, na yafuate taratibu zote za kusafirisha vifurushi hivyo" amesema Naibu Waziri Nditiye.

Amesema lazima Shirika la Posta waendelee kuimarisha huduma zao na kutoa huduma bora kwani Kuna baadhi ya mizigo ni Siri na nyingine ni Mali za Serikali na lazima zisafirishwe na shirika hilo na si vinginevyo na shirika ndilo lenye uwezo wa kusafirisha mizigo vizuri.

Aidha amefurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Shirika hilo hali iliyopelekea Shirika hilo kuondolewa miongoni mwa mashirika yaliyo katika hatari kuondolewa huku akiwataka watumishi hao kujiamini na kusema wanapoona wanakwazwa na vitu wasisite kutoa taarifa.

Pia amemtaka Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta kuhakikisha wanafungua ofisi za kubadilisha fedha katika miji yote mikuu na kuweka watu maalumu na kuhakikisha hazifungwi kwa wakati wote.

"Siku si nyingi nilikuwa na dola nikataka kubadilisha nimeenda ofisi zote nikakuta zimefungwa nikashangaa na ofisi za Posta nazo zimefungwa, Sasa nataka mkafungue ofisi kwenye miji yote mikubwa na kuhakikisha hazifungwi" amesema.

Kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe, amesema mkutano huo ni wa mwaka na huwakutanisha Mameneja wa Mikoa na watumishi wa makao makuu wanaokutana kujadili utendaji kazi na kupanga mipango mipya ya mwaka ya Shirika hilo, ambapo pia amesema wamejipanga na wameanzisha huduma kwa njia ya Mtandao kuboresha huduma hiyo.

Huku kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Kitolina Kippa amesema licha ya kazi kubwa zinazofanywa na shirika hilo bado kunachangamoto katika kwa baadhi ya Wilaya kutokuwa na ofisi za Posta.

Wakati inaelezwa kuwa Kuna ofisi za Posta 158 lakini Kuna baadhi ya Wilaya zikiwa hazina Ofisi za Posta Kama Wilaya ya Nyang'wale ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zisizokuwa na Ofisi za Posta.
 
Hakuna jema litakalofanywa na viongozi likaonekana na tija.

By the way tuliachwa holela sana, now tunatakiwa kufuata njia tunasema NO!, but mwenye haki na usafirishaji vifurushi nchini ni posta na kampuni zilizosajiliwa.
Wanajaribu kumfufua marehemu Posta aliyekufa miaka zaidi ya 10 iliyopita!
 
Tanzaniaz bana! Wanajaribu kumfufua marehemu Posta aliyekufa miaka zaidi ya 10 iliyopita!

Wabuni mbinu mpya, siyo kuturudisha analogue ya kupokea mzigo baada ya wiki tatu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Posta/ TTCL hawawezi kufufuka mpaka pale tongotongo za kubebwa na serikali zitakapowatoka na kuja kidigitali zaidi ya biashara za kiushindani, mfano mdogo tu ni kwamba toka zoezi la kuandikisha simu zetu kwa biometric system sijawahi kutana na kijana/wakala wao mtaani kitu ambacho kimenifanya nitupe hiyo SIM Card yao na kuchukua card ya kampuni inayoeleweka
 
Posta na simu,
Simu ilishindikana wakaleta kampuni za simu, imagine hadi leo tungetegemea TTCL.... jibu unalo
Usafirishaji wa barua, sasa tunamaliza kwa barua pepe au mabasi, ukitumia posta itachukua mwezi kuipata na hawakupigii simu kukuambia kama kuna barua yako,,,, ila kwa mabasi unapigiwa simu kabla hajafika kituoni, ama anakupa jina la wakala wa basi kwenye kituo hicho.....
Baadae watasema mabasi yote yawe ya serikali....
 
Posta na simu,
Simu ilishindikana wakaleta kampuni za simu, imagine hadi leo tungetegemea TTCL.... jibu unalo
Usafirishaji wa barua, sasa tunamaliza kwa barua pepe au mabasi, ukitumia posta itachukua mwezi kuipata na hawakupigii simu kukuambia kama kuna barua yako,,,, ila kwa mabasi unapigiwa simu kabla hajafika kituoni, ama anakupa jina la wakala wa basi kwenye kituo hicho.....
Baadae watasema mabasi yote yawe ya serikali....

Hawapendi sekta binafsi wainuke. Anglia mabasi mwendo wa juu 80km/h sgr 200km/h. Mbaya zaidi ni kuwa wanatumia kodi za sekta binafsi kuuwa sekta binafsi.

Haya ni kwetu tu. Kwingine sekta binafsi ni wadau si washindani.
 
Back
Top Bottom