Naibu Waziri Mwanri aibua Ufisadi wa kutisha Ludewa - Aikataa nyumba iliyofisadiwa

Ukitaka kumgusa Mwanry kwenye ujenzi weka vitasa vya UNION na Mbao za mninga!!!
 
Kilimanjaro. . . Siha.

Yuko tofauti sana na akina Basili Mramba, jamaa anachapa kazi ila wenzake tu wa juu yake ndio wanaomwangusha. Bora wampe mamlaka kuwa waziri mwenye madaraka kamili, maana anayoibua utekeleza unaweza kwamishwa na wajuu yake.
 
Yuko tofauti sana na akina Basili Mramba, jamaa anachapa kazi ila wenzake tu wa juu yake ndio wanaomwangusha. Bora wampe mamlaka kuwa waziri mwenye madaraka kamili, maana anayoibua utekeleza unaweza kwamishwa na wajuu yake.

Anajitahidi kwakweli.
Sema ndio kama unavyosema, aliyepo chini hawezi kufanikisha sawa na uwezo wake kama waliopo juu ni kazi bure.
 
DSCF8449.JPG
DSCF8461.JPG


Picha Kushoto
Ziara ya ghafla ya naibu waziri Mwanri kwenda kufichua ufisadi wa kutisha Lupanga kwa kukataa nyumba ya mganga iliyochakachuliwa ujenzi wake

Picha Kulia:
Hii ni nyumba mpya ambayo bado inajengwa ila inavuja mabati yamechakaa kabla ya kuanza kutumika ipo Lupanga Ludewa ,naibu waziri hapa akitamani kutoa machozi kwa wizi huu wa kutisha


DSCF8487.JPG
DSCF8476.JPG


Picha Kushoto:
Hii ni nyumba mpya ambayo bado haijakamilika kujengwa ila imechoka mbaya haina tofauti na pagale

Picha Kulia:
NAIBU waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na serikali za mitaa na tawala za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri amevunja ratiba iliyoandaliwa na viongozi wa wilaya ya kumtembeza katika miradi isiyo na matatizo na kuomba kupelekwa katika mradi wa ukarabati wa nyumba ya mganga wa zahanati Lupanga na kubaini ufisadi wa kutisha na kuagiza wilaya kusimamisha Mara moja ukarabati wa nyumba hiyo.
​​

DSCF8463.JPG
DSCF8472.JPG


Picha Kushoto:
Maajabu nyumba mpya ya mganga Lupanga Ludewa imechakaa kabla ya kuanza kutumika imekarabatiwa kwa Tsh,milioni 7 za serikali kupitia mradi wa Mamu
Kuta za nyumba hiyo kwa nje zikiwa zimepigwa lenda ila ndani lenda hakuna

Picha Kulia
Paa laonekana la nyumba kuu kuu ya karne iliyopita, ndo pesa za walipa kodi zinavyoteketezwa.

NAIBU waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na serikali za mitaa na tawala za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri amevunja ratiba iliyoandaliwa na viongozi wa wilaya ya kumtembeza katika miradi isiyo na matatizo na kuomba kupelekwa katika mradi wa ukarabati wa nyumba ya mganga wa zahanati Lupanga na kubaini ufisadi wa kutisha na kuagiza wilaya kusimamisha Mara moja ukarabati wa nyumba hiyo.

Naibu waziri huyo alifanya ziara hiyo leo katika wilaya ya Ludewa na kuonyesha kuwashangaza viongozi wa wilaya ya Ludewa baada ya kuivunja ratiba iliyopangwa na kuomba kupelekwa katika mradi huo ambao fedha zake kiasi cha shilingi milioni 7 zilizotengwa kukarabati nyumba hiyo kuonyesha kuchakachuliwa kutokana na mkandarasi kuezeka bati chakavu katika jengo hilo na kujengwa kuta kwa tope.

Akitoa maagizo kwa mkuu wa wilaya ya Ludewa Georgena Bundala baada ya kukagua ujenzi huo ambao mkandarasi wake Bw.Chanzy Mgaya kudai kuugua ghafla na kukimbizwa katika zahanati ya Mlangali katakana na kupata taarifa ya ugeni wa ghafla katika eneo lake la kazi .

Mwanri alisema kuwa amelazimika Kutembelea katika eneo hilou la ujenzi wa nyumba ya mganga bila ya kuwajulisha viongozi wa wilaya mapema baada ya kupokea taarifa za uchakachuaji wa kazi hiyo kutoka kwa wasamaria wema na taarifa kutoka katika ofisi za Tamisemi hivyo kulazimika kutoka eneo hilo.

Naibu waziri huyo alisema kuwa hatua ya kumwagiza mkuu huyo wa wilaya ya Ludewa na mkurugenzi kusimamisha Mara moja ujenzi huo ni baada ya kutorizishwa na kiwango cha ujenzi huo.


Alisema kasoro kubwa aliyoiona katika ujenzi huo ni jengo hilo kuja kubomoka kabla ya mganga husika kuanza kulitumia katakana na ujenzi wake kujengwa holela na kuwa mbaya zaidi nyumba hiyo inajengwa bila kuwekwa Lenda na kuwa mkandarasi huyo ameshindwa kujengwa nyumba kwa kiwango na kuwa hat a bati zinazotumika ni chakavu ambazo zimeanza kuvuja kabla ya nyumba kumalizika.

Hivyo alisema kuwa ni vema viongozi wa wilaya ya Ludewa wakachukia kwa yeye kusimamisha ujenzi wa nyumba hiyo ila fedha za umma zisitumike vibaya.

Kwa mujibu wa ratiba ya wilaya naibu waziri huyo alipaswa kapokelewa eneo la Lusitu majira ya saa 3.00 asubuhi ila naibu huyo alifika eneo hilo saa 2.23 asubuhi na kupokelewa na mbunge wa jimbo hilo la Ludewa Deo Filikunjombe na katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa Felix Haule ambao walikuwa katika msafara huo huku viongozi wa wilaya na madiwani wakifika eneo hilo na kumkuta naibu waziri huyo na msafara wake kutoka mkoani Iringa wakiwasubiri.

Pia ratiba ilikuwa ikionyesha kuwa baada ya naibu waziri huyo kukagua barabara ya Lusitu - Madilu na mradi wa umwagiliaji wa Mkiu msafara wake Ungeelekea Mlangali kukagua chumba cha upasuaji ila hakufanya hivyo aliomba msafara wake kuchepuka njiani Kwenda kijiji cha Lupanga kuona ukarabati wa nyumba hiyo ya mganga ambao katika ratiba haikuwepo.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa Monica Mchilo alimweleza naibu waziri huyo kuwa mkanadarasi huyo Mganya amekarabati nyumba hiyo kinyume na maagizo ya Baraza la madiwani na kuwa k kurudishia mabati chakavu katika nyumba hiyo.
,
Huku mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimpongeza naibu waziri huyo kuwa kufanya ziara ya katika wilaya hiyo katika kipindi hike cha masika ambacho viongozi wengi wa kitaifa huwa hawafiki Ludewa.

Kwa hisani ya Mzee wa Matukio Daima


Hamna lolote kwa huyu Mwanri..wale wale tu..sema kidogo huyu anajitambua..sio kama kaka zake werema na wassira

 
Filikunjombe majuzi tu alikuwa huko jimboni kwake, yaelekea aliona yanayojilia Na huyu naibu Waziri ni damu changa isiyoingiwa na virus. Yaelekea vijana kama hawa tukiwa nao kila mkoa mbunge mmoja na kila wizara mmoja naona wanaweza washa mwenye ukamulika zaidi.

kama huyo Filikunjombe ndo hawezi kazi kabisaa maana anafanya kazi kwa visasi mno, kwa mfano mdogo tu filikunjombe alimwagiza mwandisi kuhakikisha anampa tenda mmoja kati ya madiwani waliokuwa upande wa mr. mwaliosi wakati wa kampeni hili kuhakikisha diwani huyo anakuwa upande wake, lakini mwandisi hakutimiza hilo kwa kuwa aliona diwani huyo hakidhi vigezo vya tenda husika na hivyo basi hakaamua kuto mpa tenda akaanza kumsakama, juzijuzi hapa karumbana kweli na dereva mmoja wa hospital pale mrangali kisa alikuwa anampigia debe mr. mwaliosi na kuhaidi kummaliza dereva huyo hasa kwa kuhakikisha dereva huyo anafukuzwa kazi pamoja na mwenzake, sasa nauliza kitu kimoja kwa nini hakulizuia hili kutokea?*



* * * * * *
* "jamani wananchi wanalia mbolea za luruku mpaka leo ccm kweli mmechoka"


 
Back
Top Bottom