Naibu Waziri Mwanri aibua Ufisadi wa kutisha Ludewa - Aikataa nyumba iliyofisadiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Waziri Mwanri aibua Ufisadi wa kutisha Ludewa - Aikataa nyumba iliyofisadiwa

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Jan 17, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Picha Kushoto
  Ziara ya ghafla ya naibu waziri Mwanri kwenda kufichua ufisadi wa kutisha Lupanga kwa kukataa nyumba ya mganga iliyochakachuliwa ujenzi wake

  Picha Kulia:
  Hii ni nyumba mpya ambayo bado inajengwa ila inavuja mabati yamechakaa kabla ya kuanza kutumika ipo Lupanga Ludewa ,naibu waziri hapa akitamani kutoa machozi kwa wizi huu wa kutisha


  [​IMG] [​IMG]

  Picha Kushoto:
  Hii ni nyumba mpya ambayo bado haijakamilika kujengwa ila imechoka mbaya haina tofauti na pagale

  Picha Kulia:
  NAIBU waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na serikali za mitaa na tawala za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri amevunja ratiba iliyoandaliwa na viongozi wa wilaya ya kumtembeza katika miradi isiyo na matatizo na kuomba kupelekwa katika mradi wa ukarabati wa nyumba ya mganga wa zahanati Lupanga na kubaini ufisadi wa kutisha na kuagiza wilaya kusimamisha Mara moja ukarabati wa nyumba hiyo.
  ​​

  [​IMG] [​IMG]

  Picha Kushoto:
  Maajabu nyumba mpya ya mganga Lupanga Ludewa imechakaa kabla ya kuanza kutumika imekarabatiwa kwa Tsh,milioni 7 za serikali kupitia mradi wa Mamu
  Kuta za nyumba hiyo kwa nje zikiwa zimepigwa lenda ila ndani lenda hakuna

  Picha Kulia
  Paa laonekana la nyumba kuu kuu ya karne iliyopita, ndo pesa za walipa kodi zinavyoteketezwa.

  NAIBU waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na serikali za mitaa na tawala za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri amevunja ratiba iliyoandaliwa na viongozi wa wilaya ya kumtembeza katika miradi isiyo na matatizo na kuomba kupelekwa katika mradi wa ukarabati wa nyumba ya mganga wa zahanati Lupanga na kubaini ufisadi wa kutisha na kuagiza wilaya kusimamisha Mara moja ukarabati wa nyumba hiyo.

  Naibu waziri huyo alifanya ziara hiyo leo katika wilaya ya Ludewa na kuonyesha kuwashangaza viongozi wa wilaya ya Ludewa baada ya kuivunja ratiba iliyopangwa na kuomba kupelekwa katika mradi huo ambao fedha zake kiasi cha shilingi milioni 7 zilizotengwa kukarabati nyumba hiyo kuonyesha kuchakachuliwa kutokana na mkandarasi kuezeka bati chakavu katika jengo hilo na kujengwa kuta kwa tope.

  Akitoa maagizo kwa mkuu wa wilaya ya Ludewa Georgena Bundala baada ya kukagua ujenzi huo ambao mkandarasi wake Bw.Chanzy Mgaya kudai kuugua ghafla na kukimbizwa katika zahanati ya Mlangali katakana na kupata taarifa ya ugeni wa ghafla katika eneo lake la kazi .

  Mwanri alisema kuwa amelazimika Kutembelea katika eneo hilou la ujenzi wa nyumba ya mganga bila ya kuwajulisha viongozi wa wilaya mapema baada ya kupokea taarifa za uchakachuaji wa kazi hiyo kutoka kwa wasamaria wema na taarifa kutoka katika ofisi za Tamisemi hivyo kulazimika kutoka eneo hilo.

  Naibu waziri huyo alisema kuwa hatua ya kumwagiza mkuu huyo wa wilaya ya Ludewa na mkurugenzi kusimamisha Mara moja ujenzi huo ni baada ya kutorizishwa na kiwango cha ujenzi huo.


  Alisema kasoro kubwa aliyoiona katika ujenzi huo ni jengo hilo kuja kubomoka kabla ya mganga husika kuanza kulitumia katakana na ujenzi wake kujengwa holela na kuwa mbaya zaidi nyumba hiyo inajengwa bila kuwekwa Lenda na kuwa mkandarasi huyo ameshindwa kujengwa nyumba kwa kiwango na kuwa hat a bati zinazotumika ni chakavu ambazo zimeanza kuvuja kabla ya nyumba kumalizika.

  Hivyo alisema kuwa ni vema viongozi wa wilaya ya Ludewa wakachukia kwa yeye kusimamisha ujenzi wa nyumba hiyo ila fedha za umma zisitumike vibaya.

  Kwa mujibu wa ratiba ya wilaya naibu waziri huyo alipaswa kapokelewa eneo la Lusitu majira ya saa 3.00 asubuhi ila naibu huyo alifika eneo hilo saa 2.23 asubuhi na kupokelewa na mbunge wa jimbo hilo la Ludewa Deo Filikunjombe na katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa Felix Haule ambao walikuwa katika msafara huo huku viongozi wa wilaya na madiwani wakifika eneo hilo na kumkuta naibu waziri huyo na msafara wake kutoka mkoani Iringa wakiwasubiri.

  Pia ratiba ilikuwa ikionyesha kuwa baada ya naibu waziri huyo kukagua barabara ya Lusitu - Madilu na mradi wa umwagiliaji wa Mkiu msafara wake Ungeelekea Mlangali kukagua chumba cha upasuaji ila hakufanya hivyo aliomba msafara wake kuchepuka njiani Kwenda kijiji cha Lupanga kuona ukarabati wa nyumba hiyo ya mganga ambao katika ratiba haikuwepo.

  Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa Monica Mchilo alimweleza naibu waziri huyo kuwa mkanadarasi huyo Mganya amekarabati nyumba hiyo kinyume na maagizo ya Baraza la madiwani na kuwa k kurudishia mabati chakavu katika nyumba hiyo.
  ,
  Huku mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimpongeza naibu waziri huyo kuwa kufanya ziara ya katika wilaya hiyo katika kipindi hike cha masika ambacho viongozi wengi wa kitaifa huwa hawafiki Ludewa.

  Kwa hisani ya Mzee wa Matukio Daima
   
 2. N

  Njele JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Nymba ya mganga mkuu hii, siamini kama ni mpya labda walikosea njia? Imechoka hivi kabla hajaingia pesa imeishia wapi?
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hawa ndio mawaziri wawajibakaji lakini utaona watu wataanza kumkatisha tamaa kwa kudai anataka urais.....hongera mheshimiwa,katika serikali hii mawaziri wachapakazi mpo wawili tu..pigeni kazi watz tunayo macho na tunaona nani wafanya kazi na nani wapigo domo!
   
 4. M

  Mr Richard Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kazi nzuri anafanya mh Mwanry, kama kweli anaamini anachokisimamia basi wote wanaohusika na matumizi mabaya ya pesa ya umma wachukuliwe hatua za kisheria. Kinyume na hapo anachokifanya yataonekana maigizo mbele ya umma wa WaTZ.
   
 5. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mkuu Njele umeambiwa hii nyumba inafanyiwa ukarabati sio kujenga nyumba mpya, kama ni mpya kwa Tshs 7,000,000/= ulitegemea kukuta nyumba ya aina gani????????? Wote hao ni wahuni viongozi pamoja na wakandarasi, maanake hiyo budget inatia shaka!!!!!!!!
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii dharau sasa, siku hizi kila "mtu" anafaa kuwa Rais eeeh?
   
 7. M

  Mr Richard Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi nzuri ya MWANRY itapimwa na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wote walioshiriki ufisadi huo. Vinginevyo utaonekana mchezo wa kuigiza.
   
 8. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani mimi nadhani shida kubwa iko kwa Madiwani wetu! Hawa jamaa mimi wakati mwingine nashinwa kuelewa kazi zao! Endapo mradi unatekejelzwa, kawaida lazima iandikwe ripoti. Madiwani nao hukagua miradi na kuandika ripoti, Pia kwenye vituo husika kuna kamati za miradi. Suala la kujiuliza hapa ni je kamati ya kituo cha afya, na kamati za madiwani, pamoja na watenadaji wa halmashauri hawakuona huo huozo hadi aje Mwanri kuibua! Sijui sisi watz nani ameturoga?
   
 9. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mwanri anapambana sana,hata bukoba alifichua mengi tu,Big up mheshimiwa
   
 10. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hayo mambo ya Mh. Aggrey Mwanri yametuchosha kwani ni sawa ni mchezo wa kuigiza. Hayo mambo yameibuka Mikoa ya Mara, Kagera na Manyara na wala hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya viongozi wabadhirifu.

  Kinachoonekana ni kwamba ni yeye aonekane anafanya kazi lakini hakuna matunda yanayoonekana kwa vile ubadhirifu
  na ufisadi ni jadi ya nchi yetu.

  Kwani wabadhirifu wanalindwa.
   
 11. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  labda mkuu kama unaweza kutujuza estimate ya pesa iliyotumika mpaka sasa kwenye ujenzi huu.
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  si nilisema,huyu tayari kishaenda kwenye urais....kama nani kwa mfano huyo "kila mtu" mzee?issue hapa ni uwajibikaji wewe umeshatangulia kwenye urais,kwa hiyo watu wasiwajibike?
   
 13. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kuna taratibu na mamlaka nyie vijana sio naibu waziri tu anaamua,yeye ame play part yake mtu kama pinda na namba moja inabidi wasapoti anachokifanya ndio hatua ziweze kuchukuliwa,kama wakubwa hawawapi support hawa kina nyalandu na mwanri kila siku tutawaona wanapiga kelele tu...
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Biashara matangazo, lol!!
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Filikunjombe majuzi tu alikuwa huko jimboni kwake, yaelekea aliona yanayojilia Na huyu naibu Waziri ni damu changa isiyoingiwa na virus. Yaelekea vijana kama hawa tukiwa nao kila mkoa mbunge mmoja na kila wizara mmoja naona wanaweza washa mwenye ukamulika zaidi.
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Go Aggrey. . .
  Hayo unayofanya yafike na kule nyumbani.
   
 17. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kama Jairo na Luhanjo hawajachukuliwa hatua, unafikiri nchi hii kuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mafisadi wa vijijini?
   
 18. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hivi huyu ni mbunge wa mkoa gani vile?
   
 19. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Aggrey Mwanri ni Mbunge wa Mkoa wa Kilimanjaro - Jimbo la Siha
   
 20. i

  isoko Senior Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aggrey usiishie Kagera,Njoluma - Ludewa njoo na Kilindi Tanga ujionee madudu ya watendaji wako.
   
Loading...