Naibu Waziri: Madereva hatarishi wafutiwe leseni za udereva

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini ametoa maelekezo hayo kwa Makamanda wa Mikoa kuwafutia na kuwanyang'anya leseni madereva hatarishi ambao wamekuwa hawafuatia na kuzingatia sheria za usalama barabarani licha ya Elimu ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikitolewa na Jeshi la Polisi

Sagini amezungumza hayo wakati alipo wajulia hali baadhi ya majeruhi wa ajali iliyotokea Februari 9,2023 ambayo imesababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 36 mara baada ya basi la abiria la Kampuni ya Frester kugongana uso kwa uso na Lori lililokuwa limebeba saruji katika Kijiji Cha Silwa Pandambili , barabara kuu ya Dodoma-Morogoro.

Akizungumza na majeruhi wa ajali hiyo ambao 25 waliruhusiwa mara baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo na kuruhusiwa kuendelea na safari Sagini amewataka Wanachi kuhakikisha wanapaza sauti zao kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya mwendo kasi kwa madereva au wanapoona kusimama kwa safari mara kwa mara kutokana na ubovu wa magari wanayosafiria kwa kupiga namba za simu za Makamanda wa Polisi zilizopo ndani ya mabasi wanayosafiria

" Wadau wa usafirishaji wakiwemo madereva na sisi abiria wote Inapaswa tuguswe na mwenendo wa madereva wetu tukatae na tupige kelele. Pale unapoona dereva anaendesha kwa mwendo hatarishi kataeni kwa sababu mkinyamaza na baadhi mkishangilia wakati mwingine mnakwenda kushangilia yanayopelekea mwisho wetu. Uamuzi wa Dereva yule haukuwa uamuzi kabisa wa mtu mwenye akili za kawaida unaovertake magari mawili yote marefu na mbele mnaona kuna gari inakuja akili za kawaida zinakwambia subiri. Lakini akili zake zikamwambia nenda na abiria mmo ndani yake.”Alisema Sagini.

Sagini amewasihi Wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri kuwa vyombo hivyo vinamasharti yake kunaviwango vya spidi ya kutembea lakini pia kama unataka kupita gari nyingine lazima uwe na tahadhari ya kutosha kwani dereva aiyesababisha ajali hakuwa na tahadhari ya kutosha.
 
Mabasi yote ya abiria yanayofika kuanzia Saa 12 Jioni Dodoma yasiruhusiwe kuendelea na Safari!!

Nina experience Moja niliipata Mwaka Jana,nilisafiri na basi la Majinja kutoka Mpanda to Dar!!,Safari ilikuwa Njema kabisa huku dereva akiendesha kwa kufuata Sheria zote za barabara!!

tuliingia Dodoma Kama Saa Moja hivi,pale CBE kwanza alijaza abiria wengi Sana wengine wakiwa wamesimamishwa!,baada ya hapo huo mwendo ambao tulitoka nao kutoka Dodoma mpaka Dar,aisee ni Mungu tu nadhani alisaidia!!
 
Bado kuna udhaifu kwenye usimamizi wa Sheria za Barabarani au inawezekana Sheria zetu hazijitoshelezi, hivyo kuna haja ya kuziboresha na kuzisimamia.

Haya matukio yatapungua kwa kiasi kikubwa na hatutapoteza nguvu kazi ya Taifa letu. Kwa kuwa Kama Sheria zetu zitajitosheleza dereva hatafanya uzembe barabarani.
 
Bado kuna udhaifu kwenye usimamizi wa Sheria za Barabarani au inawezekana Sheria zetu hazijitoshelezi, hivyo kuna haja ya kuziboresha na kuzisimamia. Haya matukio yatapungua kwa kiasi kikubwa na hatutapoteza nguvu kazi ya Taifa letu. Kwa kuwa Kama Sheria zetu zitajitosheleza dereva hatafanya uzembe barabarani.
Sheria zina jitosheleza. Ila tatizo ni rushwa. Ukipita barabara ya Arusha Mbeya kupitia Dodoma, ukae mbele utaona vituko vya dereva na maaskari wa usalama barabarani,
Yaani pesa husokotewa kwenye tissue paper kama sigara, polisi akinyoosha mkono kikaratasi chenye buku mbili hudondoshwa hapo chini na safari inaendelea. Kikosi cha usalama barabarani ndio chanzo cha ajali barabarani.
 
Hii ya misokoto sio kwa njia hiyo tu. Nimeshuhudia kondakta akifunga shs elfu mbili mbili nyingi inawezana zikiwa na thamani ya shs 50,000/- . Hizi huanza kugawiwa Kibaha maeneo Kongowe mpaka unafika Manyoni. Kule mbele usiku huwa umeingia kwa hivi hakuna mbambamba, ni mwendo tu. Hii ni kwa njia ya Dar-Bukiba.
Kuhusu kujaza abiria ni jambo la kawaida kwa safari za usiku hasa kutokea Dodoma. Abiria hupangwa kwenye korido tena chini wamenyoosha miguu. Sikushtuka kusikia eti majeruhi ni zaidi ya 50 wakati uwezo wa mabasi yale ni abiria 52-55. Askari wa usalama barabarani wanajua fika kuhusu hilo. Mbaya zaidi tunaambiwa kulikuwa na askari wawili ndani ya basi.
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini ametoa maelekezo hayo kwa Makamanda wa Mikoa kuwafutia na kuwanyang'anya leseni madereva hatarishi ambao wamekuwa hawafuatia na kuzingatia sheria za usalama barabarani licha ya Elimu ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikitolewa na Jeshi la Polisi

Sagini amezungumza hayo wakati alipo wajulia hali baadhi ya majeruhi wa ajali iliyotokea Februari 9,2023 ambayo imesababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 36 mara baada ya basi la abiria la Kampuni ya Frester kugongana uso kwa uso na Lori lililokuwa limebeba saruji katika Kijiji Cha Silwa Pandambili , barabara kuu ya Dodoma-Morogoro.

Akizungumza na majeruhi wa ajali hiyo ambao 25 waliruhusiwa mara baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo na kuruhusiwa kuendelea na safari Sagini amewataka Wanachi kuhakikisha wanapaza sauti zao kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya mwendo kasi kwa madereva au wanapoona kusimama kwa safari mara kwa mara kutokana na ubovu wa magari wanayosafiria kwa kupiga namba za simu za Makamanda wa Polisi zilizopo ndani ya mabasi wanayosafiria

" Wadau wa usafirishaji wakiwemo madereva na sisi abiria wote Inapaswa tuguswe na mwenendo wa madereva wetu tukatae na tupige kelele. Pale unapoona dereva anaendesha kwa mwendo hatarishi kataeni kwa sababu mkinyamaza na baadhi mkishangilia wakati mwingine mnakwenda kushangilia yanayopelekea mwisho wetu. Uamuzi wa Dereva yule haukuwa uamuzi kabisa wa mtu mwenye akili za kawaida unaovertake magari mawili yote marefu na mbele mnaona kuna gari inakuja akili za kawaida zinakwambia subiri. Lakini akili zake zikamwambia nenda na abiria mmo ndani yake.”Alisema Sagini.

Sagini amewasihi Wananchi wanaotumia vyombo vya usafiri kuwa vyombo hivyo vinamasharti yake kunaviwango vya spidi ya kutembea lakini pia kama unataka kupita gari nyingine lazima uwe na tahadhari ya kutosha kwani dereva aiyesababisha ajali hakuwa na tahadhari ya kutosha.
Pia kampuni ambazo zina rekodi mbaya za ajali, zifutiwe leseni.

Mathalani hii kampuni ya Frester ina rekodi mvaya sana ya ajali za mara kwa mara.
 
Mapendekezo ya madereva wa kufutiwa leseni kwa Dar es salaam,njia za daladala,wanaotoka kigamboni kwenda Mkuranga na wale wanaotoka mwandege kigamboni, tukiweza kuanza na hao itakuwa salamu tosha kwa wale wa basi za mkoa🤔
 
Udereva unachangiwa na tabia ya mtu kama ilivyo kwenye shughuli zingine tu,

Discipline and attitude,haya mambo mtu anafundishwa toka utotoni,nchi kama Japan na Singapore wamefanikiwa kwenye hili,

Adhabu ya kufungiwa leseni naiunga mkono,kosa la kwanza warning kisha kosa la pili afutiwe leseni ila ijulikane ni makosa yapi hasa ndio Dereva anaweza kufutiwa leseni?
 
Mapendekezo ya madereva wa kufutiwa leseni kwa Dar es salaam,njia za daladala,wanaotoka kigamboni kwenda Mkuranga na wale wanaotoka mwandege kigamboni, tukiweza kuanza na hao itakuwa salamu tosha kwa wale wa basi za mkoa🤔
Njia ya Dar- Tunduma, waanze na Newforce/Golden Deer na Sauli. Haiwezekani basi lifike Uyole saa 11.30 jioni.
Labda turudi enzi zile za Tawaqal na M-Sleeping Coach.
 
Kuna wakati kama na kumbuka vizuri nilipanda new force nikienda mbeya,nilisema sipandi tena lile gari,ila walionisikia wakasema ni kawaida ya gari za uelekeo ule,kwani wafanyabishara wengi wanahitaji kuwahi,hivyo wapo tayari kumwona dereva ili wawahi mambo yao, 🤔
 
Kuna ile DPK 912. Hawa jamaa ni balaa.
 
Back
Top Bottom