Naibu waziri kilimo watesa familia zetu

makamaka

Member
Dec 1, 2011
55
28
Mheshimiwa Bashe,

Mbona watesa familia za watanzania wenzako wanyonge,ulipokuwa kiongozi wetu wa New habari (2006) ltd ulilazimisha tupewe barua za kupunguzwa kazi bila idhini yetu na kutuahidi kutulipa fedha zetu za retenchment na malimbikizo ya mishahara yetu kwa wiki mbili.

Ilikuwa mwezi wa sita na sasa ni October inaenda november hakuna taarifa yeyote.
Kumbuka watanzania wenzako tena wanyonge tupo mtaani tunahaha kutafuta kazi na hakuna chochote cha kusapoti familia zetu.

Tunajua una majukumu makubwa ya Taifa hili lakini hili linakuhusu kwa asilimia zote.tunakuomba utushughulikie malipo yetu tuachane kwa amani kiongozi wetu.

Tunakuomba uvae viatu vyetu na ulitizame swala hilo kwa mtazamo mkubwa ulionao.Nadhani unajua wazi namba moja wetu hapendi watu wake wadhulumiwe.

Tunakusihi sana rekebisha hili ili nafsi yako iwe safi na uwendane na uwajibikaji wa seikali ya awamu hii.

Asante.
 
Back
Top Bottom