Naibu Waziri Kakunda: Binti hatoolewa bila 'leaving certificate' ya form four

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251


Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda amewatahadharisha Viongozi wa dini nchini kujihadhari na kuwaozesha wasichana ambao hawajamaliza elimu ya kidato cha nne ili kuwakamata wazazi wote wanaoshiriki kuwaozesha watoto wao kwasababu ya kupewa mimba wakiwa masomoni.

Amesema kuwa watoto wa kike wanashindwa kumaliza masomo kwasababu ya mimba ama kuozeshwa jambo ambalo limeendelea kuisumbua serikali katika juhudi zake za kuokoa maisha ya watoto wa kike ili waendelee na masomo na kuongeza kuwa Wilaya ya Nkasi kuna tatizo sugu la mimba kwa kuwa na mimba 152 kati ya 325 kwa Mkoa mzima.

Amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini sana maisha ya watoto wa kike na inaendelea kuweka mikakati ya kila namna ili kuhakikisha kuwa wasichana hao wanapata elimu stahiki, kwa kuanza na elimu bure na kuendelea na mikakati ya marekebisho ya sheria kadhaa ili watoto wa kike waendelee na masomo.

“Haiwezekani mtu anatakatisha fedha hapati dhamana, halafu mtu anampa mimba mwanafunzi na kisha anapata dhamana, tunakoelekea ili uolewe lazima uwe na “leaving Certificate” ama tujue kuwa hukusoma kabisa ili tuwahoji wazazi, mwananfunzi ambae ataolewa kwa kukatishwa masomo kamata wote na funga miaka 30, wazazi wa pande mbili, aliyeoa, aliyeolewa, wanaoshangilia, aliyefungisha ndoa wote miaka 30 jela,” alifafanua.

Aidha, amewashauri wanaharakati kuungana pamoja katika kuwaelimisha watoto wa kike na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha mimba zinapungua na kuwa vitendo hivyo haviendelei, ili kuwainua watoto wa kike kielimu.
 
Ni wa kuwasamehe hawa jamaa

Yaani leaving certificate anadhani ni kama vitumbua kwamba kila mtanzania anayo

Hawa jamaa naona kama tumewaazima mahali au nchi fulani. Hawajui uhalisia wa maisha ya watanzania kabisa
 
Hivi kuna wanahrakati waliishtaki serikali na kuishinikiza ifanyie marekebisho sheria ya ndoa. Mwanasheria mkuu si ndo aliweka pingamizi akakata rufaa ili isifanyiwe marekebisho? Au mwanasheria mkuu alitokea chausta? Hawa jamaa huwa wanavuta kitu gani?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom