Naibu Waziri Hamisi Kigwangalla akutana na Viongozi wa taasisi za wazee kutoka mikoa ya Tanzania

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipowapokea viongozi wawakilishi wa taasisi za wazee kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Hawa ni viongozi wa shirikisho la vyama vya wazee nchini (Tanzania Older People's Platform - TOP). Wazee walimshukuru Mhe. Rais wa JMT, Dkt. John Pombe Magufuli na serikali yake kwa kazi nzuri wanayofanya kuleta mabadiliko ya kweli nchini, na zaidi kwa kuanzisha wizara maalum yenye kushughulikia mambo yao.

Na pia walimpongeza Mhe. mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli kwa kuifanya ajenda ya wazee kuwa ni ajenda yake ya kudumu. Wazee pia walitaka kujua nini vipaumbele vya serikali ya awamu ya tano kwenye mambo ya wazee.

Dkt. Kigwangalla alielezea kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka vipaumbele kwenye maeneo makubwa mawili, nayo ni pensheni ya wazee, bima ya afya bure kwa wazee, na kutunga sheria ya wazee na kutengeneza mkakati maalum wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wazee, kuwaelimisha kuhusu shughuli za uzalishaji mali na kuwawezesha.

Mhe. Waziri Mkuu alielekeza kuwa pamoja na kuyafanyia kazi mambo hayo, ni lazima wizara ianzishe mchakato wa kutafuta namna ya ya kuanzisha utaratibu wa kutenga pesa kwa ajili ya mfuko wa wazee kwenye halmashauri zote nchini, kama ambavyo wanawake na vijana wanapataa, iwe ni kwenye kubadili fomula ya kuigawa ile 10% ya vijana na wanawake ama ni kutenga 15% kwenye kila halmashauri, pia kuweka utaratibu mzuri wa kuwatambua wazee na kuwajengea uwezo wa kujiajiri wenyewe na pia kuwapatia ulinzi wa kisheria na kuelimisha jamii kuhusu haki za wazee.
3221ad07eafc94e26c04f12dd7963b55.jpg
9c3f4f38ed6614620d6745dd6eb18a3c.jpg
30a2dd906f722d91911afe1fe860000b.jpg
3ec73449f5bb46c841b508af514a49d8.jpg
 
Back
Top Bottom