Naibu waziri elimu awasimamisha watumishi nane wa VETA Pwani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Ukiukwaji wa taratibu katika kutunuku zabuni za upatikanaji mafundi jamii wa ujenzi wa chuo cha VETA Rufiji umepelekea kusimamishwa kazi kwa watumishi nane wa chuo cha VETA Pwani ambao walikuwa katika Kamati ya ujenzi wa chuo hicho.

Hatua hiyo imefikiwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa chuo hicho leo ambapo aligundua kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa kutunuku mafundi ujenzi kupitia force akaunti uliopelekea ujenzi wa chuo hicho kuzorota.

“Kuanzia leo nawasimamisha kazi wote waliokuwa kwenye Kamati ya ujenzi na nawaagiza Takukuru kuwafanyia uchunguzi ili kubaini kilichofanya wakakiuka utaratibu kwa kiwango kikubwa hivi,” amesema mhe. Kipanga.

Kamati hiyo ya ujenzi yenye jumla ya watu nane ilimtunuku fundi jamii mmoja aliyejulikana kwa jina la Phillipo Urasi, zabuni ya kujenga majengo 16 kinyume na utaratibu unaotaka fundi mmoja kupewa zabuni ya kujenga jengo moja tu.

Aidha, mhe. Kipanga amemsitisha fundi huyo kuendelea na ujenzi na kuagiza wachaguliwe mafundi wengine mara moja kutoka kwenye orodha ya wazabuni waliotuma maombi awali ili kazi iweze kumalizika kwa wakati.

“Naagiza pia huyo fundi Urasi asimame kazi kuanzia leo na nataka Mkurugenzi wa VETA Makao Makuu usimamie kuhakikisha wanapatikana mafundi wengine haraka, kutoka kwenye orodha ya mafundi walioomba kazi mwanzo ili kazi iendelee na kukamilika kwa wakati uliopangwa,” amesisitiza Mhe. Kipanga.

Akisoma taarifa ya ujenzi, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Pwani, Clara Kibodya amesema kuwa mpaka sasa wameshapokea jumla ya Sh. Bilioni 1.1 na kwamba ujenzi mpaka sasa umefikia asilimia 33 na unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi Machi mwaka huu.

Waliosimamishwa kazi ni Leonard Mwandumbya Mwalimu wa Umeme,

Aibu Issa Mwalimu wa Maabara, Haji Sinani Mwalimu wa majokofu na viyoyozi, David Thobias Mwalimu wa Magari, Erasto Thomas Mwalimu wa useremala na msimamizi wa ujenzi, Tumaini Magina Mwalimu wa Electronics, Paul Kimaro Mwalimu wa Engineering Science na Kubri Mkwanda Afisa Manunuzi
 
Hivi hawa TAKUKURU kwa nini wasianze kuchunguzwa wao kujua wanazembea wapi kufanya kazi yao? Maana ukisoma habari za ubadhirifu wa mali ya umma lazima uone maagizo kwa takukuru kuchunguza taasisi husika.

Hao TAKUKURU hawaoni wenyewe ubadhirifu mpaka waagizwe? Na hapo watu wamesimamishwa kazi, si lazima majibu ya takukuru yatakuwa positive kutomshusha kuaminika/ hadhi naibu Waziri.
 
Urasi au Urassa?
 
Baba ame- budget kwamba kilo hamsini za mchele zitatosha kwa matumizi ya familia ya mwezi.
Baba anamtuma dogo dukani kununua hizo kilo hamsini.
Dogo ana- negotiate na muuzaji: "Pima kilo 38, risiti andika kilo 50"
Mambo yanaendelea. Baba yuko comfortable kabisa.
Tarehe 20 ya mwezi mchele umeisha. Baba hana habari, yuko glosari pembeni akiburudika na angalau kabia kamoja.
Ghafla mama anatokea, mwiko mkononi: "Angalia sasa baba nanihii, jitu zima umekalia mambo ya ulevi hata hujui kwamba nyumbani mchele umekwisha. Utakua lini? " Mbele za watu. Daa! Baba hata haelewi, kichwa kinamuuma. Kila akijitahidi kufanya awezavyo kuitunza familia yake anayoipenda sana, badala ya shukrani, ni dharau na matusi, tena hadharani!
Anawaza afanyeje dunia hii? Machizozi yanamtoka polepole kwa huzuni kali ya moyo!.
Anaacha bia yake nusu na kurudi nyumbani.
 
Hivi hawa TAKUKURU kwa nini wasianze kuchunguzwa wao kujua wanazembea wapi kufanya kazi yao? Maana ukisoma habari za ubadhirifu wa mali ya umma lazima uone maagizo kwa takukuru kuchunguza taasisi husika.

Hao TAKUKURU hawaoni wenyewe ubadhirifu mpaka waagizwe? Na hapo watu wamesimamishwa kazi, si lazima majibu ya takukuru yatakuwa positive kutomshusha kuaminika/ hadhi naibu Waziri.
Takukuru hawawezi kuwa kila mahali. Wanafanyia kazi taarifa wanazozipata ama kwa intelijensia au tuhuma zinazofikishwa kwao kwa namna mbalimbali ikiwamo maagizo ya viongozi.
 
Lakini viongozi wanaweza kuwa kila mahali? Yaani Waziri atoke Dodoma mpaka Mtwara aibue uozo na kuagiza TAKUKURU waliopo Mtwara wafanye uchunguzi, unaona jambo la kawaida. Au hiyo kutokuwa kila mahali unamaanisha nini mkuu?
 
Back
Top Bottom