Naibu Waziri azozana na nduguye hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Waziri azozana na nduguye hadharani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by armanisankara, Oct 20, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk.Charles Tizeba amedaiwa kuingia katika kashfa ya kutaka kupigana na kaka yake wakiwa katika baa moja jijini Mwanza.

  Dk.Tizeba amedaiwa kutaka kupigana na kaka yake huyo aitwaye Adrian Tizeba Jumatatu iliyopita katika baa moja inayofahamika kama Nyanguli Pub ambako pia huuzwa chakula cha asili ya wakazi wa kanda ya ziwa (ugali wa mhogo kwa samaki).

  Akisimulia kuhusiana na mkasa huo, Tizeba (Adrian) ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Lugata wilayani Sengerema alisema kwamba siku hiyo majira ya kati ya saa 8:00 na saa 9:00 alasiri akiwa Jijini Mwanza alikwenda katika baa hiyo kwa lengo la kupata chakula akiwa na wenzake wawili.

  Aliwataja wenzake hao kuwa ni Joseph Mwita ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Isamilo Jijini Mwanza na mtu mwingine aliyemtaja kwa jina moja la George ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chadema wilaya ya Nyamagana.

  Alidai kuwa wakiwa hapo ghafla alitokea Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk.Tizeba ambaye baada ya kuwaona alikwenda katika meza yao kwa lengo la kuwasalimia na alianza kumsalimia George kisha akamsalimia Mwita kwa kushikana mikono.

  Hata hivyo Tizeba ambaye alijiuzulu udiwani na kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutimkia Chadema, aliendelea kudai kwamba kisha Dk.Tizeba alinyoosha mkono kutaka kumsalimia yeye (Adrian), lakini aligoma kumpa mkono kwa sababu wamekuwa katika mgogoro kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

  “Hapa lazima niwe mkweli, alipomaliza kuwasalimia wenzagu niliokuwa nao ndipo akataka kunisalimia na mimi, lakini nilimgomea kwa sababu mimi na yeye (Dk.Tizeba) hatuna maelewano na hatujasalimiana wala kuwa na mawasiliano kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa,” alisema.

  Kwa mujibu wa Tizeba, mbali na kumkatalia salaam alimtaka pia Dk.Tizeba aondoke awapishe ili waendelee na mazungumzo yao.

  Hata hivyo alidai kuwa badala yake Dk.Tizeba aligoma kuondoka huku akimhoji kaka yake huyo kwamba asipoondoka atamfanya nini.

  “Wenzangu niliokuwa nao pia walimsihi aondoke, lakini alipoanza kuondoka ghafla akageuka kurudi kwa lengo la kupigana baada ya kuwa nimemwambia kwamba anajaribu kufanya usanii mbele za watu ili ionekane tuna uhusiano mzuri wakati si kweli,” alisema.

  Aliongeza kwamba Dk.Tizeba alipogeuka kurudi naye (Adrian) alisimama kwa lengo la kujihami, lakini wenzie aliokuwa nao waliingilia kati na kuwazuia wasifanye kitendo hicho cha fedheha hadharani.

  Mmoja wa watu waliokuwepo na kushuhudia tukio hilo, Mwita alikiri kuwa tafrani hiyo ilitaka kutokea, lakini walijitahidi kuwazuia ndugu hao wa damu wasipigane hadharani.

  “Ni kweli siku hiyo majira ya saa tisa hivi tulikuwa pale Nyanguli Pub na Tizeba (Adrian) tukiwa tunaendelea na mazungumzo alikuja mtu mmoja ambaye baadaye nilitambulishwa kuwa ndiye Naibu Waziri wa Uchukuzi (Dk.Tizeba) kwani ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuonana naye ana kwa ana,”alisema Mwita.

  Aliongeza kwamba ni kweli baada ya kuingia na kuwaona wamekaa watatu katika meza moja, Dk.Tizeba alikwenda kuwasalimia, lakini alipotaka kumsalimia kaka yake aligoma na ndipo wakaanza kurushiana maneno makali.

  Mwita ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema wilaya ya Nyamagana alisema kwamba miongoni mwa maneno aliyoyasikia yakitamkwa na Dk. Tizeba kumwelekea kaka yake ni pamoja na “Unadhani nakuogopa, unacheza na mimi, utashindwa tu tutaona,”alisema.

  Alibainisha kwamba kimsingi alisikitikia hali hiyo hasa kwa vile wahusika ni watu wazima wenye akili timamu na zaidi mmoja ni kiongozi wa serikali ambaye hakupaswa kuonyesha hadharani tofauti iliyopo baina yake na kaka yake.

  Alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani, Dk.Tizeba bila kukanusha wala kukiri kuhusika katika tukio hilo alimuonya mwandishi wa NIPASHE kwamba asijitumbukize katika njama za kutaka kumchafua.

  “Sikiliza wewe, kabla hata sijasema chochote nataka nikuonye, ukijitumbukiza katika kampeni ya kunichafua hatutakuwa marafiki,” alionya Dk.Tizeba.

  Aliongeza kwamba anavyofahamu yeye kama kweli kaka yake huyo angekuwa amefanyiwa fujo kama anavyodai angekwenda polisi na siyo kwenye vyombo vya habari.

  “Anayefanyiwa fujo anakwenda polisi, wewe si polisi, ungemwambia aende polisi, kwani nyinyi huwa mnasuluhisha migogoro? Hebu achana na hayo,” alisema Dk.Tizeba.
   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,106
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Siasa zinavunja hadi undugu???!!!!
  Duh
   
 3. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo ya kifamilia yanatuhusu nini hapa?
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Viongozi wetu wengi wanahitaji msaada mkubwa jinsi ya ku-behave na hasa namna ya ku-deal na media. Jinsi huyu Naibu waziri alivyomjibu mwandishi wa habari, ingekuwa kwenye nchi za wenzetu kesho kibarua chake kingeota majani. Badala ya kujibu swali, naibu waziri anatoa vitisho! Na hii iko kila mahali hadi wakubwa wa polisi. Hawajielewi kabisa.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  eti kwani wamesikia binadamu hawagombanagi
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  duh, ila inaonekana kaka ana lake, ya nini undugu wa familia kuuleta kwenye vyombo vya habari?

  Anajiona hana la kupoteza.
   
 7. M

  Mwanamutapa JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 499
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Dk Tizeba si mstaarabu hata kidogo kukosana na kaka yake haishangazi ni mtu anayependa kujikuza sana ndio maana aliposhinda mchuano ndani ya CCM mwaka 2005 kamati kuu hawakurudisha jina lake badala yake walirudisha Chitalilo ila kwa sababu ni swahiba wa Kikwete alibahatika kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Sikonge katika mkoa wa Tabora.

  Ni mtu mjanjamjanja mwenye kujikuza na kupenda kunyeyekewa sana na ni mtu wa rushwa ndio maana alifukuzwa kazi na Magufuri alipokuwa mhandizi wa mkoa wa Mwanza sababu ya kuruhusu kujengwa kwa kituo cha mafuta kwa njia ya rushwa kituo kikajengwa eneo lisilo ruhusiwa pona yake ya kurudi barabarani alisaidiwa na Jk baada ya kuwa mshabiki mkubwa wa Jk 2005 na kusikika akisema CCM isipomchagua Jk wananchi wa Mwanza hawataridhika na mgombea yeyote na kwasababu Jk ni mpenda misifa alimpokea Tizeba kwa mikono miwili pasipokujali kuwa ni mfujaji wa mali za umma

  Kibaya zaidi anapenda kutongoza wake za watu pia wanafunzi wa sekondari kwa kutumia uwaziri na hupenda kumtumia mdogo wake ambaye ni mfamasia kwa taaluma kuchukua namba za simu za mabinti tena kwa kulazimisha juzijuzi kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa wilaya wa CCM na mjumbe wa NEC katika wilaya ya Sengerema alionekana kutongoza wajumbe wa CCM waziwazi kwa kutuma wapambe zake bila kujali umri wao maana wengine walionekana kwa umri kuwa wadogo mara tatu yake lakini yeye kwa kujua ni naibu wziri aliwataka kwa nguvu bahati nzuri wengi walimkataa bila kujali uwaziri wake. Mtu mzima lakini hovyo
   
 8. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,077
  Likes Received: 4,662
  Trophy Points: 280
  No news....
   
Loading...