Naibu Waziri ataka Taasisi za Dini na Serikali kukomesha mauaji nchini

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Naibu waziri wa fedha na Mipango , Hamad Chande amezitaka taasisi za dini hapa nchini kudumisha ushirikiano na serikali ili matendo maovu yakiwemo mauaji yanayoendelea hapa nchini yakomeshwe.

Aidha amewataka viongozi wa dini kuzidisha nguvu katika kuijenga jamii kiroho ili iwe na hofu ya mungu kwa kuwa viongozi wa dini ni mhimili muhimu katika maendeleo ya nchi .

Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki jijini Arusha, wakati alipohudhulia harambee iliyoandaliwa na taasisi ya dini ya Kiislamu ya Twarika kwa lengo la kuchangia kutunisha mfuko wa taasisi hiyo.

Chande alisema kuwa lazima jamii imrudie mungu na kuachana na matendo maovu jambo litakalosaidia kupungua kwa uovu na ya kikatili nchini.

"Viongozi wa dini ni muhimili mkubwa sana ambao tunawategemea katika maendeleo ya nchi yetu kwa sababu wao ndio wanailea jamii na kuijenga jamii kwa imani na kitoho ili kuacha matendo maovu yanaopeleke uharamia katika nchi yetu " alisema

Aidha chande aliipongeza taasisi hiyo kwa hatua kubwa inayoifanya kwa kushirikiana na serikali katika kuhamasisha suala la sensa nchini.

Aliitaka taaisis hiyo kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kudumu na kuahidi kugharamia fenicha zote za ofisi hiyo

Katika hatua nyingine naibu waziri alitoa wito kwa viongozi wa madhehebu ya dini kuhakikisha wanashiriki vema katika kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la sensa linalotarajia kuanza agosti 23,mwaka huu lenye maslahi ya taifa na maendeleo binafsi kwa jamii.

Awali kiongozi wa taasisi ya Twarika nchiji, sheikh Haruna Husein alisema kuwa harambee hiyo inalenga kutunisha mfuko wa taasisi hiyo pamoja na kununua samani za ofisi.

Hata hivyo alisema kuwa taasisi hiyo haina ofisi ya kudumu na kuhitaji msaada ili kuweza kujenga ofisi ya kudumu.

Ends..

20220423_125644.jpg
699245291.jpg
 
View attachment 2200046View attachment 2200047
Kuijenga jamii kiroho ili iwe na hofu ya MUNGU!!! 🤔🤔🚶🚶🚶🚶🚶🚶
 
Back
Top Bottom