Naibu Waziri asema Bima ya NHIF haina madaraja, Kikao cha Bunge Julai 6, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959

NAIBU WAZIRI: HAKUNA MADARAJA KATIKA BIMA YA NHIF
Mbunge Aida Joseph Khenani alitoa hoja kuwa Wananchi wanapokata Bima za Afya za NHIF wanawekewa ukomo wa baadhi ya huduma na dawa wanapofika Hospitali hali inayofanya baadhi waone hakuna umuhimu wa kuwa na Bima hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amejibu kuwa “NHIF hakuna madaraja labda amechanganya na CHF ambapo ndipo kuna madaraja.”

MIKOPO YA SANAA MAOMBI YA TSH. BILIONI 9.2, IMETOLEWA YA TSH. BILIONI 1
Serikali imesema kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ulipokea maombi ya mikopo yenye thamani ya Tsh. 9,262,096,578 (Bilioni 9.2) kutoka kwa waombaji 219.

Hadi Aprili 2023 mikopo iliyotolewa ni ya Tsh. 1,077,000,000 kwa miradi 45 kutoka maeneo mbalimbali ya Sekta ya Utamaduni na Sanaa. 33.

Akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Mwaka 2023/24 ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema jumla ya ajira 21,579 zikiwemo 733 za kudumu na ajira za muda ni 20,846

Aidha, Mfuko umekuwa kichocheo kikubwa kwa wadau katika eneo la urasimishaji kwani umewahamasisha kurasimisha shughuli zao katika mamlaka mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Halmashauri pamoja na mamlaka nyingine za udhibiti ili waweze kuendesha shughuli zao kibiashara.
 
Kiufupi hakuna faida ya bima kwa mwananchi tatizo linakuja hatuna vipato endelevu vitakavyofanya tuweze kigawa pesa kwenye kila tunachohitaji. Hebu fikiria yule mtu aliepo kijijini hana hospitali wala kituo cha afya kizuri hata akiwa na bima itamsaidia nn kama hatuna huduma bora.

Bima iwe hiari na wasiipigie debe sana kama ni kitu muhimu kwa wananchi tunajua ni miradi yao lakini kwetu haina faida inatuumiza tu kijinga. Kama wanataka waweke mifumo itakayofanya bima imnufaishe mtu na si kumnyanyasa. Ushapimwa unaambiwa dawa kanunue na unakuta duka halipokei kadi ya bima yaani ni tafrani tupu kwa mwananchi
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Watawala wanatudharau sana. Kuna vifurushi vyenye hadhi tafauti. Pia kuna waajiriwa wa serikali na mashirika. Hawa wako juu ya wachangiaji binafsi hata wanapolipa chini ya wanacholipia wasio waajiriwa.
Kisha kuna wateule. Wabunge.
 
Usimuamini mwanasiasa hata siku moja!
Mie ndio maana mule mjengoni huwa naona ni kusanyiko la genge fulani janja janja tu mradi mkono uende kinywani!.
 
.
Screenshot_20230522_130203_com.android.chrome.jpg
 
Na speaker amesikiliza na kukuukubali huu uongo bila yu kuomba ufafanuzi? Kama hawa watu wanaweza kudanganya mbele ya kadamnasi kama Bungeni wapi watasema ukweli ???
 
Amejibu ndivyo sivyo,, NHIF kuna kadi za Blue kwa daraja la chini na kadi za Green kwa daraja la juu aache uongo wake.
 
Kadi za bima za mfanyakaz wa BOT, TRA, TPDC ni tofauti na mfanyakazi wa Halmashauri
 
Na speaker amesikiliza na kukuukubali huu uongo bila yu kuomba ufafanuzi? Kama hawa watu wanaweza kudanganya mbele ya kadamnasi kama Bungeni wapi watasema ukweli ???
Labda Speaker alisinzia. Mana si fix ile
 
  • Thanks
Reactions: vvm

NAIBU WAZIRI: HAKUNA MADARAJA KATIKA BIMA YA NHIF
Mbunge Aida Joseph Khenani alitoa hoja kuwa Wananchi wanapokata Bima za Afya za NHIF wanawekewa ukomo wa baadhi ya huduma na dawa wanapofika Hospitali hali inayofanya baadhi waone hakuna umuhimu wa kuwa na Bima hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amejibu kuwa “NHIF hakuna madaraja labda amechanganya na CHF ambapo ndipo kuna madaraja.”

MIKOPO YA SANAA MAOMBI YA TSH. BILIONI 9.2, IMETOLEWA YA TSH. BILIONI 1
Serikali imesema kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ulipokea maombi ya mikopo yenye thamani ya Tsh. 9,262,096,578 (Bilioni 9.2) kutoka kwa waombaji 219.

Hadi Aprili 2023 mikopo iliyotolewa ni ya Tsh. 1,077,000,000 kwa miradi 45 kutoka maeneo mbalimbali ya Sekta ya Utamaduni na Sanaa. 33.

Akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Mwaka 2023/24 ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema jumla ya ajira 21,579 zikiwemo 733 za kudumu na ajira za muda ni 20,846

Aidha, Mfuko umekuwa kichocheo kikubwa kwa wadau katika eneo la urasimishaji kwani umewahamasisha kurasimisha shughuli zao katika mamlaka mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Halmashauri pamoja na mamlaka nyingine za udhibiti ili waweze kuendesha shughuli zao kibiashara.

Wanadamu tuwe na shukrani. NHIF wametuwekea Vifurushi na kila mtu anajipimia kulingana na mahitaji yake kama vifurushi vya simu vile.

Zamani kulikuwa na aina moja unachangia karibu milioni hata kama mtu mmoja sasa hii ya vifurushi ndo pona yetu.

Mi nina kifurushi cha Najali Afya na kwa kweli kinanifaa na familia yangu

Sasa niulize kidogo pia Kwani aina za uanachama ni madaraja? Maana mtu anajiunga kulingana na mahitahi yake na ukubwa wa familia mi sioni shida

Lakini We unajisajilije bila kujua unapata nini? Kwa nini huulizi kabla hujajisajili?
 
Naibu waziri amedanganya madaraja yapo bima ya mbunge inamtibu mpaka nje ya nchi ... Lakini ya mtumishi wa umma ataishia MNH tu ... Iweje aseme haina madaraja ... Katika mawaziri mzigo wa mama molel kwenye afya hatoshi ... Yaani sometimes ukimuangalia kama vile hajielewi ?! Kama issue mnahitaji Dktr awe naibu mbona mnao wabunge wengi wanaojielewa na ni madactari wa binaadam.. muondoe Kigwangalla kwani hajawahi ku practice
 
Back
Top Bottom