Naibu Waziri amkaanga Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ulanga

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
4.jpg


Naibu Waziri wa Maji amchukulia hatua za kinidhamu Mhandisi Ulanga

Muungwana Blog 5 · 49 minutes ago

[https://4]


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amechukua hatua za kinidhamu kwa Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Interconsult kutokana na kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Gombe uliopo Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri ameagiza vyombo vya usalama kumkamata na kufanya uchunguzi kwenye mradi huo wa Gombe ambao umechelewa kukamilika licha ya asilimia kubwa ya fedha kuwa zimeshalipwa kwa mkandarasi, lakini pia unakosa thamani halisi ya fedha zilizotumika katika ujenzi wake.

Aweso alitoa maagizo hayo wakati alipokuwa ziarani katika Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro mara baada ya kupata taarifa ya kusuasua kwa mradi huo na wananchi wa Gombe kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.

‘‘Katika taarifa nimeambiwa kuwa mradi unatoa maji, lakini nimekuja kuona na si kweli wakati wizara imetoa fedha.

Kama Naibu Waziri wa Maji sitakubali kusikia fedha za miradi ya maji zinaliwa kila ninapoenda, naagiza Mhandisi Mshauri akamatwe na uchunguzi ufanyike na endapo itabainika amehujumu achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wahandisi wote nchini’’, alisema Aweso.

Amesema kuwa wizara itaandaa orodha ya majina ya wakandarasi wote waliohujumu miradi ya maji na kuikabidhi kwa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi ili wafutiwe kabisa usajili na kutopewa kazi yoyote tena nchini endapo watathibitika kufanya hivyo.

Akiwa Ulanga Naibu Waziri Aweso amezindua ofisi ya maji ya Kata ya Lupiro, mradi wa maji wa visima 27 katika Kijiji cha Chikuti, ambacho ni moja ya vijiji vinavyonufaika na mradi huo na kukagua skimu ya umwagilaji ya Mnepa, iliyopo Kata ya Lupiro.
 
Ripoti inasema mradi unatoa maji...kwenda site hakuna kitu.

Ndiyo maana kuna watu wanasema wanammiss JK kwa ajili ya mambo kama haya.
 
Back
Top Bottom