Naibu Waziri akiri maeneo mengi ya taasisi za serikali hayajapimwa, wananchi wamevamia na kujenga makazi

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amekiri kuwa maeneo mengi ya umma hayajapimwa na yamekuwa chanzo cha kuvamiwa na wananchi wasio na nia njema lakini amezitaka taasisi hizo kupima na kumilikishwa ardhi hiyo ili yatumike kwa matumizi yaliyokusudiwa.

“Maeneo ya shule, soko, zahanati, vituo vya afya, hospitali, vyuo, vituo vya polisi, mahakama, maeneo ya Jeshi, hifadhi ya misitu na maeneo ya makumbusho hutengwa maalumu kwaajili ya matumizi ya umma na shughuli mbalimbali za serikali. Maeneo yote hayo yako chini ya usimamizi na uangalizi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa au Serikali Kuu”,

“Hata hivyo maeneo mengi kati ya hayo yamekuwa yakisimamiwa na taasisi za serikali bila kupimwa wala kuwa na hati miliki badala yake yamekuwa yakimilikishwa kwa kupewa ‘Government allocation’. Utaratibu huu umekuwa ukitoa mwanya kwa wananchi wenye nia ovu kuyavamia, kuyamega maeneo ya serikali kinyume na utaratibu”

Changamoto hiyo imeibua migogoro ya mara kwa mara baina ya wananchi na serikali katika matumizi ya ardhi, ambapo wananchi hao wamekuwa wakipata hasara kwa kulazimishwa kuondoka katika maeneo hayo ambayo wanauziwa na baadhi ya watendaji wa serikali kinyume na sheria.

Waziri Mabula amesema “Serikali kupitia Wizara yangu iliagiza maeneo yote ya umma yapimwe na kumilikishwa kwa taasisi husika. Nitoe rai kwa wakuu wote wa taasisi za umma kuhakikisha wanakamilisha zoezi hili mapema”

Hata hivyo amewataka watu waliovamia maeneo ya serikali kuondoka mapema kabla zoezi la kuwaondoa halijaanza ili kuwaepusha na usumbufu na hasara ya mali zao.

“Kwa maeneo ambayo yamevamiwa ni vema wavamizi wakaondoka kwa hiari yao na wasisubiri mkono wa sheria uwakumbe”, amesema Waziri Mabula.

Zaidi, soma hapa => Waziri akiri maeneo mengi ya taasisi za serikali hayajapimwa, wananchi wanavamia na kujenga makazi | FikraPevu
 
hayo maeneo kama yamechukuliwa na raia wa tanzania hilo sio tatizo, tatizo ni serikali kutoyaendeleza hayo maeneo....
 
Back
Top Bottom