Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
Naibu Waziri wa kazi, vijana na Ajira ,Mhe Anthony Mvude amefanya ziara ya kikazi katika Makao makuu ya mtandoa wa simu ujulikanao kama Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es salaam .
Mavude alipata nafasi ya kukagua vibali vya kuishi nchini pamoja na vibali vya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wa kigeni wanaofanyia kazi katika kampuni hiyo ya matandao wa simu wa Vodacom Tanzania.
Halikadhalika Naibu waziri alifanya ziara hiyo kwa kutaka kujua kero na maendeleo mbalimbali ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ila kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.
Mnama tarehe 30 Desemba mwaka jana Naibu Waziri alitembelea Makao makuu ya Tigo ya yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujitosheleza kwa jinsi gani inaajili waajiri wake, katika zaira hiyo alibaini mambo kadhaa ambayo angependa kampuni ya Tigo ivifanye.
Katika maswala ya afya na usalama na pia ingependa kuona mikataba baina ya Tigo na watoa huduma wake, nakusema serikali ya awamu ya tano ipo makini kuhakikisha sheria inafuatwa na inayozingatia sheria.
Vodacom ni kampuni bora yenye mtandao we uhakika Nchini na hutumiwa na watu wengi zaidi Mjini na vijijini wakiwa na kauli mbiu yao isemayo “VODACOM KAZI NI KWAKO”.