Naibu Spika wa Bunge wa zamani Mathias Michael Kihaule afariki dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Spika wa Bunge wa zamani Mathias Michael Kihaule afariki dunia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 5, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  NA MUHIBU SAID

  5th June 2012

  Naibu Spika wa Bunge wa zamani, Mathias Michael Kihaule, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.

  Kwa mujibu wa taarifa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, jijini Dar es Salaam iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, alifariki Jumapili ya Mei 3, mwaka huu.

  Kihaule ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Ludewa, mkoani Iringa, alizaliwa Julai 19, 1933 na amefariki akiwa na umri wa miaka 79.

  Licha ya kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15, kuanzia mwaka 1980-1995, Kihaule alilitumikia taifa katika wadhifa wa Naibu Spika wa Bunge.

  Alikuwa na wadhifa huo katika kipindi chake cha tatu cha ubunge, kuanzia mwaka 1990 mpaka mwaka 1995.

  Baada ya kipindi chake cha ubunge, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, kuanzia mwaka 1995 hadi 2004.

  Katika utumishi wake wa umma, Kihaule amewahi pia kushika nyadhifa kadhaa kitaaluma, ikiwamo Mkufunzi wa Vyuo mbalimbali vya Ualimu nchini.

  Hadi alipofariki, alikuwa akijihusisha na shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji, na atakumbukwa na wananchi wa Ludewa kwa jinsi alivyokuwa akishirikiana nao katika maendeleo ya jimbo na wilaya yake kwa kipindi chote alichokuwa bungeni na mara baada ya kumaliza muda wake wa ubunge.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa mtoto wake, Dk Anold Kihaule, Ilala Maghorofani, ambako ibada ya kuaga mwili itafanyika leo Msimbazi Centre kuanzia saa 6 mchana, kabla ya kusafirishwa kesho kwa ndege kwenda Ludewa kwa mazishi.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin.

  CHANZO: NIPASHE


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Poleni ndugu na Marafiki wa familia...
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Poleni wanafamilia sie wote tu waja wake Mungu!
   
 4. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Poleni sana wafiwa wote.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  ???????

  !!!!? Sielewi mie
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,948
  Trophy Points: 280
  hana picha?
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,948
  Trophy Points: 280
  ndio waandishi wetu hao usishangae sana anajua bado tuko mwezi wa tano..like kindergaten ..
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  "
  Hadi alipofariki, alikuwa akijihusisha na shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji, na atakumbukwa na wananchi wa Ludewa kwa jinsi alivyokuwa akishirikiana nao katika maendeleo ya jimbo na wilaya yake kwa kipindi chote alichokuwa bungeni na mara baada ya kumaliza muda wake wa ubunge."

  Tanzania siyo sehemu ya kufanya kazi; miaka 79 bado jembe; jembe na yeye kutumika kote huko hakuwa na akiba ya kumfanya apumzike?

  RIP Mathias
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Rest In Peace Naibu!

  Hata picha ccm hawajampigaga??

  ccm janga kwa Taifa letu!
   
 10. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  R I.P katuombee ufisadi uishe tz huko utakapokuwa.
   
Loading...