Naibu Spika wa bunge la 11 na UKAWA

dizzle1

Member
Jan 16, 2011
85
9
Awali ya yote ningependa kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mh Dr Tulia Ackson Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Tanzania kwa namna anavyo ongoza bunge letu hili la 11.

Baada ya uteuzi wake watanzania walio wengi walikuwa na hofu juu ya utendaji wake katika bunge hili ambalo 60% ni vijana,ni bunge ambalo litakuwa na changamoto kubwa sana ukilinganisha na mabunge yaliyo pita. Kwa muda huu mfupi toka achaguliwe Dr Tulia Mwansasu ameonyesha ueledi mkubwa sana wa kuliongoza bunge letu,kwa dhati kabisa chama chetu cha UPDP kina mpongeza tena kwa umahiri mkubwa wa uongozi alio uonyesha.

Chama chetu cha UPDP kina penda kuelezea kwa masikitiko makubwa kwa namna ambavyo vyama vinavyo unda umoja wa UKAWA kususia vikao vya bunge kwa sababu nyepesi kabisa kuwa aviridhishwi na utendaji wa Kiti cha Naibu Spika Dr Tulia Ackson,chama chetu kwenye hili kina ungana na watanzania walio wengi wanao laani vikali kitendo hiki kisicho na uungwana na kama kitaendelea kuvumiliwa kitaenda kuwa gawana watanzania kwa misingi ya siasa za hovyo kabisa zinazofanywa na viongozi wa UKAWA.

Hili bunge liendeshwe kwa ueledi kiti cha Spika kina paswa kuheshimiwa,bunge haliwezi kuendeshwa kwa matakwa ya wanasiasa pekee. Wanasiasa hawawezi kuwa juu ya kiti cha Spika,lazima kiti cha spika kieshimiwe hili tuwe na uhuru wa kutoa michango ya maoni,mawazo yetu,fikra zetu na uwazi wa kuwasilisha kwa hoja zetu bila ubaguzi au takwa la kundi fulani la wanasiasa.

Kwa kuhitimisha,chama cha UPDP kina penda kuweka msimamo wake wazi juu ya hatua ya UKAWA kutoka bungeni kuwa ni maamuzi ya hovyo kabisa yaliyo wai tokea toka tumeingia mfumo wa vyama vingi,tena yasio heshimu wananchi walio wachagua kwenda kuwawakilisha bungeni.

UPDP kina toa raia kwa wanachama,wapenzi,wakereketwa, wanaharakati na watanzania wote wanao penda kuishi katika amani iliyohasisiwa na wazee wetu na tawala zilizopita kuwapuuza viongozi wa UKAWA na kulaani vikali misimamo ya namna hii yenye lengo la kutaka kuugawa umma wa watanzania.

Imetolewa leo;

Felix Marcus Makuwa

Naibu Katibu Mkuu Taifa

Chama cha United People Democratic Party
 
Dr Tulia anazidi kupata watetezi. UKAWA waendelea kuweka mpira kwapani
 
UPDP...ni chama gani hivi ? ni tawi la ccm pale lumumba au ? mtu hata mwenyekiti wa kitongoji hana kwenye nchi hii...na bado hiv vyama shirika vya ccm ndo vitazikwa kabisa.....
 
Kuna chama kinaitwa UPDP?? ha ha ha, hivi ndivyo vyama vinavyopendwa nchi hii, Vyama ambavyo hata havijulikani, lakini vikitoka hadharani vinakemea vyama vingine vya upinzani. Vyama tiifu na dhaifu, na vinavyopata asilimia 0.01 ya kura katika kila uchaguzi. CCM inapenda sana vyama vya namna hii, na inatamani nchi yetu iwe na vyama vyote vya upinzani vyenye kufanana na hiki.
 
Back
Top Bottom