Naibu Spika Job Ndugai ana matatizo gani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Spika Job Ndugai ana matatizo gani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Aug 5, 2011.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Job Yustino Ndugai, Naibu Spika na Mbunge wa Kongwa.
  • Ahoji uadilifu wa baadhi ya watendaji serikalini, kutokana na tabia yao ya kuvujisha siri za Serikali kwa wabunge wa upinzani.
  • Awaomba wabunge wa CCM kuisaidia Serikali kupitisha bajeti kwani kutofanya hivyo ni kuwaongezea nguvu wapinzani bungeni.
  Ikumbukwe kwamba hizi anazodai ni siri za serikali ni pamoja na;
  • Nyaraka zinaoonesha wizara zikitoa hongo kwa Wabunge wa CCM ili bajeti zao zipite.
  • Nyaraka zinazoonesha pesa zikilipwa kwenye akaunti binafsi kununua Shirika la Umma.
  • Ushahidi kuonesha Wabunge wa CCM wakipewa hongo ili halmashauri mbali mbali zisiwajibishwe.
  • .............................. na kashfa nyingi tu zinazolikumba Taifa kila leo.
  Hii ina maana kama Job Yustino Ndugai angekuwa na uwezo katika kipindi kilichopita 2005 - 2010, kashfa kama za EPA, Kagoda, Kiwira, Dowans, Meremeta, Rada angewawajibisha waliovujisha hizo anazoita siri za serikali.

  Halafu bila aibu ni huyu huyu Ndugai aliyeongoza ujumbe wa Wabunge nchini Uingereza eti kwenda kufuatilia aliyoita chenji ya rada huku akidai nchi hii inaheshimika kwa uadilifu na matumizi bora !

  Job Yustino Ndugai anadai ni heri kashfa zikafagiliwa chini ya kitanda kuliko Upinzani kupata nguvu kwa kutetea maslahi ya Taifa. Je tumweleweje huyu Naibu Spika na Mbunge wa Kongwa, kwa nini alitaka awe mwakilishi wa watu wa Kongwa?

  Job Yustino Ndugai hawaonei hata huruma wananchi wa Kongwa wanavyoendelea kuteseka kwa umaskini na maradhi kwa sababu ya huu mfumo fisadi ?
   
 2. franksarry

  franksarry JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 1,107
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160

  Ni mtu wa mzahaa tuu (Joti wa the comedy original is more serious na kazi yake).
  He is not a serious politician n man of a word!

  Ameanza vituko, Nadhani amegundua udhaifu wa Boss wake wa kushindwa kuwa Mzungumzaji mzuri ktk vikao vyao vya wabunge wa CCM,
  So anajitahidi 2015 ampige bao but hataweza kufanikiwa....!
  Haya ndiyo matokeo ya siasa uchwara...
  Hizo siasa zitawamaliza kabla ya 2015!,
  maana huo mwaka 2015 bingwa wao wa mchezo uchafu R Az hatakuwepo amejitoa jumla na CCM, bahati iliyomwangukia Bi A Makinda 2010 haitakuwepo....!
   
 3. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watu kama hawa wanastahili madaraka yao kuishia kwa familia zao tu
   
 4. tama

  tama JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 604
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya kanyanganeni wenyewe kwa wenyewe tuu.
   
 5. p

  plawala JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kilaza
  Ni mnafiki
  Ni kuwadi wa ufisadi

  Sifa hizo anazo kwa mtiririko huo toka juu mpaka chini,Huyu dawa yake ni kumtafutia mgombea wa upinzani makini 2015

  Atakuwa mpiga kura wa kawaida baada ya hapo
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Je, kwa kuhoji uadilifu wa baadhi ya watendaji serikalini eti kwa sababu wana tabia yao ya kuvujisha siri za Serikali kwa wabunge wa upinzani tumweleweje ?
  • Kwamba watendaji wa serikali wafumbie macho uhalifu ?
  • Kwamba watendaji wa serikali hawatakiwi kuwa waaminifu ?
  • Kwamba watendaji wa serikali watangulize itikadi maofisini ?
  • Kwamba watendaji wa serikali wawalinde viongozi mafisadi ?
  • Kwamba kwa watendaji wa serikali uadilifu una maana tofauti ?
  Je, kwa kuwaomba wabunge wa CCM kuisaidia Serikali kupitisha bajeti kwani kutofanya hivyo ni kuwaongezea nguvu wapinzani bungeni tueleweje ?
  • Kwamba jukumu lao kuwa bungeni ni kuilinda na kuitetea serikali ?
  • Kwamba wanatakiwa kutanguliza maslahi ya chama mbele ya taifa ?
  • Kwamba hawatakiwi kuwawajibisha watendaji serikalini wanapoboronga ?
  • Kwamba wasithubutu kukwamisha hoja inayowasilishwa bungeni na serikali ?
  • Kwamba wasikubaliane na Upinzani hata kama wana hoja zenye maslahi kwa taifa ?
  Msimamo kama huu wa Job Yustino Ndugai kama mbunge na Naibu Spika ni kielelezo halisi cha ulimbukeni wa wabunge wa CCM. Hivyo ndivyo walivyo na haijalishi kama ni kilaza kama Lameck Airo wa Rorya au msomi kama Andrew Chenge wa Bariadi, wote wanaogelea kwenye dimbwi hilo hilo chafu. Ndugu zangu tuamke la sivyo hawa walafi watatumaliza, hawashibi - wamezaliwa katika ufisadi, wamekua katika ufisadi, wanaishi katika ufisadi na watakufa katika ufisadi.
   
 7. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hakutarajia kuwa naibu spika, ndio maana hajiamini¨¨

  cha kusikitisha analazimisha siasa,,,,,,mijitu ya namna hii ingekuwa kanda ya kaskazini wangekuwa wanausikia tu ububge wanatumia ujinga wa wapiga kura wao
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mjomba, inawezekana akawa both mnafiki na pia kuwadi wa mafisadi na nilianza kumjua pale alipokwenda London kudai pesa za Radar na kuojiwa na Mtangazaji wa BBC kuhusu hatua walizochukuliwa watuhumiwa wa Tanzania, wakati Tanzania nzima inawajua watuhumiwa wa sakata la Radar kwa maana wengine walijiuzulu hadharani na kuachia uwaziri, JOB NDUGAI alidai kutowafahamu kabisa hao watuhumiwa wa radar.nilichanganyikiwa sikuamini masikio yangu ilinibidi niende nikasilikilize tena yale mahojiano lakini nikagundua kuwa sikukosea alisema yeye hawajui hao watuhumiwa wa Radar.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Naibu Spika anaendekeza ukada wa chama, si angetafuta kazi ya chama tujue moja.

  Ofisi ya Speaker ina integrity beyond party politics, this buffoon does not understand or appreciate that.

  Kichwa cha thread ni "Naibu Spika Job Ndugai ama ni mnafiki na kuwadi wa ufisadi au kilaza wa kutupwa"
  Inawezekana kabisa yote kweli.
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ana matatizo ya saikolojia...maana kuacha mke na kuolewa na ji mama saizi ya mama yako ni laana!!anaweweseka na laana huyo angepumzika tu hajui analofanya wala analotetea
   
 11. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is more than serious mkuu.
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukiwa na empty head inabidi uwekeze kwenye kujikomba. Hata hivyo ni aibu iliyoje kwa mwanaume mzima kama Ndugai kulamba miguu ya wanaume wengine? Hivi hii kauli aliyotoa y akuficha madhambi ya serikali ingewafikia wale waingereza aliokuwa anawaeleza kuwa bunge linaweza kusimamia change ya Radar watamuonaje?
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa hana kosa,hii inatokana na upeo wake mdogo wa kufikiri!!!
   
 14. n

  ngoko JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  inaonesha ukishaitwa kada wa chama tawala uwezo wako wa kufikiri unauacha nyumbani kwako na badala yake unakuwa unazungumza vitu bila kujali kama vinakujenga au kukubomoa kwa mwanvuli wa ' maslahi ya chama '
   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Spika kapigiwa kura na wabunge wa chama, hivyo si ajabu kwamba analinda masilahi ya chama hicho, bila kujali athari kwa taifa.
   
 16. V

  Vonix JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Moja kati ya mambo ambayo katika katiba mpya itabidi yasikosekane ni hili la kuwa na spika na naibu wake kuwa wa chama fulani,mi nakubaliana na wote mliochangia hapo juu Ndugai analamba miguu ya mafisadi,uwozo wa kufikiri ni mdogo sana,ni mwoga,anatabia ya kujikomba kwa viongozi wake,ni ushahidi tosha kuwa hajiamini.
   
 17. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ana kazi ya kushabikia magamba wakati jimboni kwetu hakuna maendeleo yoyote kwa muda wote wa uongozi wake jimboni Kongwa,jambo jema kwa wakati huu wananchi wa jambo hili uelewa umekua mkubwa sana ngoja tusubirie 2015
   
 18. Mchelle

  Mchelle Member

  #18
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  naunga mkono hoja, wananchi tuamke viongozi kama hawa, hata watoto wao ukiwauliza unataka kufanya kazi gani baadae atakuambia kazi ya "FISADI" unategemea mtu kama huyo atashiba?
   
 19. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #19
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafisi nilikuwa bado cjamfaham Ndugai anasimama upande gani, ila baada ya ule mdahalo wa siku ile (Lissu vs Ngugai) nikamfaham kumbe ni mnafiki na kuwadi mkubwa wa ufisadi, hasa pale alipojihapiza kwamba wabunge wote wa tz wakiwa bungen wanatanguliza chama kwanza then jimbo lake na mwisho taifa;
  wakati ukwel anaufaham kwamba magamba ndo chama mbele kwa kila kitu, Taifa mwisho.
   
 20. N

  Njaare JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Ni mbunge ambaye kwa miaka 15 ya ubunge wake amekuwa akiamini kuwa yeye ni serikali na yuko tayari kufanya lolote alimradi aifurahishe serikali. Hajafanya lolote kwa wananchi wake wanaokabiliwa na na njaa, uhaba wa maji na barabara.

  Laiti wapigakura wake wangekuwa kama wale wa mbozi wangeshamng'oa. Mbozi walipogundua kuwa Mheshimiwa Eliakimu Simpasa hakuwa anawatetea bungeni waliamua kumtosa wakampa mwingine. Simpasa naye kama ndugai aliacha alilotumwa akajigeuza serikali akaanza kuwahukumu wenzake.

  Mama Makinda hapati usaidizi wowote toka kwa ndugai zaidi ya kumharibia.
   
Loading...