Naibu Spika Job Ndugai amtoa nje Mbunge wa CCM kwa siku tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Spika Job Ndugai amtoa nje Mbunge wa CCM kwa siku tatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Jul 12, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni Faustine Ndugulie mbunge wa Kigamboni. Tulizoea kuona wa CHADEMA tu lakini leo tunamuona na wa CCM.

  Nimewahi kuwalletea thread maana nimekikuta hicho kitendo ignawa mwanzo wake sikuwepo kwenye TV.

  Ndugai katumia kanuni 73{3}:{ Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha Mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano}
   
 2. r

  richone Senior Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mbunge wa kigamboni ametolewa nje na naibu spika Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake aliyoambiwa aifute kauli yake kwamba waziri amewahonga madiwani.
   
 3. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Baada ya asubuhi kushindwa kutumia kanuni za Bunge dhidi ya Mnyika na ushahidi wake , jioni hii amethibitisha kuwa amejifunza baada ya kusoma kanuni na kazisoma tena kinyume kwani amemtoa nje Ndungulile kwa siku tatu wakati akijua wazi kuwa kanuni zinaelekeza kitu gani.


  Nanukuu kanuni za Bunge 1. Kanuniya Adhabu : hii ni kanuni ya 73 (3) "Endapo mbunge yeyote atatakiwakuthibitisha ukweli wa jambo au suala alilolisema Bungeni na hadi kufikiamwisho wa muda aliopewa amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo,Spikaanaweza kumsimamisha Mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vitano"

  Ndungulile hakuambiwa athibitishe , ila aliambiwa awaombe radhi sasa kitendo cha kumtoa nje ni kutaka kuaminisha umma kuwa hata wabunge wa CCM wanaweza kutolewa nje na hivyo yuko fair.

  kanuni ya 71 (1) "bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 100 na 101 ya KATIBA ,mtu yeyote asiye Mbunge ambaye atajisikia kuwa amepata athari hasi kutokana na kauli au maneno au shutuma zilizotolewa Bungeni kumhusu yeye binafsi ,anaweza kupeleka malalamiko pamoja na maelezo yake ya kujitetea kwa Spika:"


  kanuni 71 (2)" mara baada ya kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwake kwa mujibu wa fasili ya (1) ya kanuni hii na kujiridhisha kuwa malalamiko hayo yameandikwa katika lugha ya heshima na ya kistaarabu na yanatoa hoja mahususi na ambayo si ya uzushi ,uongo,uchochezi au chuki binafsi;na kwamba yanastahili kufikiriwa au kufanyiwa kazi na kamati ya haki,maadili na madaraka ya Bunge ,Spika atayapeleka malalamiko hayo kwenye Kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge ili kuyatafakari na kulishauri Bunge"
   
 4. Root

  Root JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,239
  Likes Received: 12,953
  Trophy Points: 280
  amesema kwa vikao vitatu na sio siku tatu.
  Ila nadhani leo amefata sheria na itakuwa fundisho
   
 5. M

  Majasho JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Halima Mdee kituko: Ndugai
   
 6. W

  Welu JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Kamtoa nje kwa siku 3 mbunge wa kigamboni katoa maneno machafu kwa Mdee eti wayu wa kawe wmechagua kutuko na hana adabu. Ooo nimechoka.
   
 7. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bunge letu limisha kuwa kama ze comedy
   
 8. K

  KASIANI Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kwel maamuz ya viongozi we2 yanachekesha. Kubwa 2subir 2015.
   
 9. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakika Bunge hili kwa ukada huu, kwani Ndungulile alisema kuwa madiwani wa Kigamboni waliletwa bungeni na waziri na hiyo ni rushwa ili waweze kukubaliana naye kuhusu mradi wa mji mpya Kigamboni ambao umewafanya wananchi washindwe kujenga kutokana na kukosekana kwa fidia na kuzuiowa kuendelea na ujenzi.

  Badala ya Ndugai kumpeleka Ndungulile kwenye kamati ya maadili anampa adhabu bila kumpa nafasi ya kujitetea , mbona hakupewa siku saba kuonyesha jinsi ambavyo waziri alikuwa amewahonga madiwani hao wa Kigamboni?
   
 10. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Kazi kweli mwaka huu hili Bunge Kariakoooo kweli
   
 11. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,805
  Likes Received: 2,749
  Trophy Points: 280
  Wa sisiem katolewa nje? Sijawahi onaga kama ya leo!
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tatizo hiyo jamii ya akina ndugai wabishi sana. wabishi hata wasichokijua
   
 13. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Amewahonga kwa lipi?
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  The statement is not clear!can you please explain more!otherwise you will be tarnishing the good image of our forum!
   
 15. Munambefu

  Munambefu JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 895
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  huyo siyo muheshimiwa naibu spika ni muishiwa spika
   
 16. r

  richone Senior Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  amewahonga kwa kuwaleta hapa bungeni Dodoma ili wakubali wananch wao wahamishwe bila ya kufanyika kwa tathimini mpya baada ya ile kupitwa na wakati.
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  At least now you have made me rough!
   
 18. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Baada ya kushindwa kutoa uthibitisho kuhusu serikali kuhonga madiwani wa Kigamboni! Wakati naibu spika akitoa hukumu ndipo Halima Mdee (waziri kivuli wa ardhi) akataka kutoa taarifa, Job Ndugai akamzuia kisheria! Ndipo akawaambia wana Kawe kuwa wamechagua kituko! Eti anataka amtoe nje apate umaarufu na aandikwe kwenye magazeti!
  My take: Job Ndugai hongera kwa kuua CCM! Janga la taifa
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama madiwani waliletwa bungeni kwa gharama za waziri/serikali ili kuwa sehemu ya mjadala ambao ki-msingi unaegemea upande wa serikali basi hiyo ni rushwa. Kama mtakumbuka ile CCCC iliyoleta kasheshe uchukuzi hadi Omar Nundu akaondolewa ofisini imekuwa black-listed kwenye miradi inayofadhiliwa na World Bank kwa sababu ya rushwa. Na aina ya rushwa ya hawa CCCC ni kama hii ya madiwani kwamba walikuwa wanawasafiirisha officials ambao ndio wanatakiwa kufnaya maamuzi.

  Nadhani matokeo ya hii adhabu ya huyu mbunge yanaweza kusaidia kumulika wageni wanaoletwa bungeni wakati wa vikao. Kuna rushwa kubwa sana.
   
 20. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Hahaha!washenzi sna,hawana maana yeyote mjengoni ccm.
   
Loading...