Naibu Spika Dkt. Tulia: Jesca Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,810
Mbunge Kishoa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amelalamikia kunyimwa nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa kabla hajaondolewa kwenye chama chake. Naibu spika akalazimika kuingilia kwa kusema haihitaji kuwa naye bungeni kama hana chama cha Siasa kwani ni takwa la kuwemo bungeni.

"Mheshimiwa Naibu spika sitaki sana kubishana na kiti chako lakini niseme mimi ni miongoni mwa wahanga wakubwa sana wa suala hili la mikutano ya hadhara, nikiwa kama katibu mkuu wa Baraza la wanawake CHADEMA wakati huo kabla sijaondolewa kwenye chama changu...'' Alisema Kishoa

Spika alimkatisha na kusema, "Mheshimiwa Kishoa hii kauli yako either uifute, ofisi ya spika haina hiyo taarifa ya wewe kuondolewa kwenye chama chako, kama umeondolewa kwenye chama chako usingekuwa humu ndani kwa sababu wabunge waliokuwemo humu ndani wote wana vyama vya siasa ndivyo katiba yetu inavyosema na ndiyo katiba yetu inavyosema ile katiba hairuhusu mbunge ambae hana chama"

Kishoa: Mheshimiwa Spika hatujaondolewa kwenye chama, bado mimi ni mwanachama wa CHADEMA kwasababu tuko kwenye taratibu na tumekata rufaa na taratibu zinaendelea

Tulia: Mheshimiwa ngoja, waheshimiwa wabunge taarifa rasmi za Bunge ni kumbukumbu, umezungumza kabla ya sentesi yako ya sasakwamba kabla hujaondolewa kwenye chama chako, futa hiyo kauli kwanza halafu umalizie mchango wako kwasababu ndani ya bunge hili tutakuwa tunavunja katiba kama tutakuwa na wewe humu kama umeshaondolewa na chama chako

Kishoa: Mheshimiwa naibu spika nimefuta

Hoja ya Mbunge Jesca ilianzia kwenye haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na kukumbana na miongozo mingi kutoka kwa wabunge wakimtaka afute kauli. Kishoa amesema nchi ikiongozwa kwa matamko badala ya katiba itapotea.

Akifafanua kuhusu mikutano ya vyama vya kisiasa, Naibu spika amesema mikutano hiyo ipo kwenye katiba za vyama vya siasa na hufanyika kwa vipindi na sio ya hadhara akitolea mfano mkutano mkuu wa CCM uttakaofata utafanyika JK Convection centre na huo ndio unaitwa mkutano wa CCM lakini Rais akienda mahali unakuwa mkutano wa Rais na si CCM.



MY TAKE:

Je, CHADEMA haijatarifu bunge kuhusu kuwavua uanachama Wabunge 19 wa CHADEMA?

Zaidi soma: John Mnyika amuumbua Spika kwa kutoa ushahidi wa Ofisi ya Spika kupokea barua ya CHADEMA kuwavua ubunge wanachama wake
 
Mbunge Kishoa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema amelalamikia kunyimwa nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa kabla hajaondolewa kwenye chama chake. Naibu spika akalazimika kuingilia kwa kusema haihitaji kuwa naye bungeni kama hana chama cha Siasa kwani ni takwa la kuwemo bungeni
Covid-19 italisumbua sana bunge.
 
Mbunge Kishoa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema amelalamikia kunyimwa nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa kabla hajaondolewa kwenye chama chake. Naibu spika akalazimika kuingilia kwa kusema haihitaji kuwa naye bungeni kama hana chama cha Siasa kwani ni takwa la kuwemo bungeni
Kishoa ushaambiwa huwa chama humo sepa !! Nchi hii ina vituko aisee..huwezi amini. Huyo mwingine na yeye aliyetolewa gelezani usiku wa manane kuwahi saa mbili asubuhi kuuapia Ubunge - katulia as if nothing illegal happened.
 
Mbunge Kishoa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA amelalamikia kunyimwa nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa kabla hajaondolewa kwenye chama chake. Naibu spika akalazimika kuingilia kwa kusema haihitaji kuwa naye bungeni kama hana chama cha Siasa kwani ni takwa la kuwemo bungeni
Covid19 ni wabunge wa Ndugai. Na Ndugai yupo juu ya Katiba. So, wacha waendelee kula mema ya nchi.
 
tusubirie mama akisharuhusu mikutano ya kisiasa,twone watavaa jezi za chama kipi wasimamapo majukwaan
Ukiitwa na Rais wa nchi ni LAZIMA uende, ila kukubaliana naye si lazima - mnaweza kushidwana vilevile na maisha yakaendelea. So wapinzani nendeni mkamsikilize hakuna dhambi yoyote ile - tunajua bado mna MACHUNGU mengi ila kwa kuwa yeye ni MAMA basi anaelewa yote mliyotendewa na serikali yake iliyopita - anaweza kuwafuta MACHOZI na mkaanza episode mpya pamoja kwa ushirikiano for the better of our nation.
 
Tulia endelea kuwafanganya wananchi. Halima mdee kwà mfano 2025 anaelekea wapi? Na kwà chama gani?au utampa jumbo la mbeya mjini? Halima bado ni mdogo kwà umri na hana ajira nyingine ataelekea wapi? Bora uwaeleze mapema kuwa hawana chama ilinwaanze kuhipanga kisiasa na kimaisha. Wengine waanze kuolewa au la.
 
Mikutano wa Rais kusiwe kunakuwepo wavaa madera ya kijani, t-shirt za kijani na kofia kama vile mikutano ya chama.
 
Back
Top Bottom