Naibu Spika Dk. Tulia Akson hakunaga. Uwezo wake wavuruga akili za wabunge wote wa UKAWA

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Sijapata kuona Kambi nzima ya Upinzani wakishikwa pabaya na wakashikika kama wakati huu. Ukiona mwanaume mzima analia mchana kweupe basi ujue kashikwa pabaya. Ukiona timu inaweka mpira kwapani badala ya kupambana uwanjani ni dhahiri kwamba mpinzani wao kawazidi uwezo. Ndivyo inavyotokea kwa Kambi ya Upinzani ikiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Nashawishika kuamini kwamba, ndani ya kambi ya upinzani, hakuna mbunge hata mmoja mwenye uwezo wa kujenga hoja za kupambana na Dr Tulia.

Kinachonifurahisha, huyu mama hakika hana papara. Yaani katulia Tuliii hali inayowafanya wana UKAWA washindwe kabisa kupambana naye. Hawa wana UKAWA walikuwa wanamuonea sana Mama Makinda. Sasa wamepata kiboko yao na hakika wanachapika sana na wataendelea kuchapika mpaka mwaka 2020 na baada ya hapo wataendelea kuchapika kwani Dr Tulia ndiye atakayekuwa Spika wa Bunge lijalo.

Binafsi nilijuwa dhahiri kwamba ikiwa Bunge litaongozwa na mtu mwenye weledi wa kanuni kama Dr Tulia Akson, ni dhahiri kwamba Upuuzi, jeuri, kejeli, dharau na kila aina ya uozo bungeni vitapotea. Hii inajidhihiri sasa. Wapinzani wanaona kuwa kila wanachofanya kwa makusudi kwa lengo la kupindisha kanuni, Dr Tulia anawanyoosha na wananyoosheka. Ndo maana wapinzani sasa hawana namna nyingine ya kukabiliana naye zaidi ya kutoka bungeni na pengine kuamua kuwa mabubu.

Hakika nampongeza sana huyo aliyemuibua Dr Tulia Akson. Ametuletea mtu sahihi kwa wakati muafaka. Wapinzani watapata shida sana kwa miaka hii mitano kwani kila watakapoingia bungeni watakutana na Dr Tulia katulia Tuliiiii hali itakayowafanya waendelee kuweka mpira kwapani kwani uwezo wa Tulia umezidi vichwa vyote vya UKAWA.

Nimalizie kwa kusema kuwa, HILI GEMU HALIHITAJI HASIRA. Mbowe na Kambi yenu endeleeni kuwa na hasira mwisho wa siku mtavuna mlichopanda.
 
Wapinzani tutapoteana sana Bungeni. Dr Tulia hakika katushika pabaya. Kama wewe ni mchezaji wa mpira wa miguu, hivi uliwahi kupigwa na mpira kwenye nyeti zako? Vipi maumivu yake? Ndivyo inavyotokea kwa wabunge wetu wa UKAWA sasa. Dr Tulia anatutandika kweli. Hatuna ujanja tena. Hata Lissu tuliyekuwa tunamtegemea kapwaya sana wakati huu
 
Daa, huyu binti katumwa kazi na anaifanya kwa ukamilifu wake, ukiona wanaume tena nguli wa siasa kama kina Mbowe, Zitto na Lissu wanapiga kelele ujue sio mchezo, naskia wameweka mpira kwapani sasa wanakwenda kumushitaki kwa raia!
 
Wapinzani tutapoteana sana Bungeni. Dr Tulia hakika katushika pabaya. Kama wewe ni mchezaji wa mpira wa miguu, hivi uliwahi kupigwa na mpira kwenye nyeti zako? Vipi maumivu yake? Ndivyo inavyotokea kwa wabunge wetu wa UKAWA sasa. Dr Tulia anatutandika kweli. Hatuna ujanja tena. Hata Lissu tuliyekuwa tunamtegemea kapwaya sana wakati huu
Duh,yaani uwezo wako wa kufikiri ndo umehitimisha kwamba Tulia anaendesha bunge kwa uwezo?Hujui yule amewekwa pale na serikali ili kuilinda serikali isivuliwe nguo?
 
Back
Top Bottom