Naibu Spika ampa onyo kali Anatropia Theonest kwa kumvua baraghashia Goodluck Mlinga

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,959
Naibu spika wa Tanzania amelifanyia kazi malalamiko ya mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga wa CCM kuvuliwa balaghashia na mbunge Anatropia Theonest wa CHADEMA na kumsababishia mfadhaiko na mtikisiko wa mawazo mbunge huyo.

Tukio hilo limeangaiwa kwenye kamera za bunge na kuonekana kweli mbunge huyo alimvua kofia.

Naibu spika amesema ni kweli tukio hilo halikubaliki na mbunge huyo wa CHADEMA alifanya kosa kubwa kikanuni kwa kusababisha fujo na dharau kwa bunge lakini kwa kuwa sheria za bunge hazijaweka adhabu kwa matendo kama hayo, ametoa onyo kali kwa mbunge huyo na akirudia basi adhabu kali zaidi itatolewa.



hapa mbunge mlinga akiwakilisha malalamiko yake
 
Wangetunga sheria na adhabu kwanza si wako peke yao, halafu ndiyo wangetoa adhabu ili wananchi tuzidi kumfahamu vizuri tulia
Sasa na wewe, nae Tulia ana kosa gani kwa ufedhuli wa huyo Theonista? Ina maana angemuadhibu, ukawa mngeendelea kukaa nje ya bunge sio? Kweli hamueleweki.
 
Sasa na wewe, nae Tulia ana kosa gani kwa ufedhuli wa huyo Theonista? Ina maana angemuadhibu, ukawa mngeendelea kukaa nje ya bunge sio? Kweli hamueleweki.
Mimi kwa mtazamo wangu naona tuko more judgemental na objective hasa tunapotoa michango yetu kwenye suala hili. Hili tukiliangalia suala hili kwa undani utakuta ni subjective kwa maana kwama Mbunge Milinga na Anathropia wanafanyakazi office moja (BUNGE). Kufanyakazi ofice moja mara nyingi huwa tunachukuliana kuwa ni familia moja. (hata kama tuko department tofauti- hapa naongelea wao wana tofauti za itikadi za kisiasa). Tunajua maisha ya watoto wa familia moja wanavyoishi. Kuna matani, kuna kutofautiana n.k. Haya yote yanatokea sehemu yoyote mahala pa kazi. Mie kwa Mtazamo wangu hawa ni watu wanaofahamiana vizuri na yawezekana wamezoea kutaniana. Ndio maana ukiangalia wakati Milinga anaomba muongozo kuhusu suala hili, body language yake ilikuwa hata inaongesha kukerwa na kitendo hicho achilia mbali maneno aliyoongea. Mie kwa Mtazamo wangu alitaka tu kuwafurahisha wabunge wenzie wajue nini kimetokea, au kwa vile ni mtu anayependa kuongea sana, hivyo alitaka tu kuwashirikisha wenzake. Kwa hiyo hata naibu speaker siamini kama hajui vitu kama hivi (utani kati ya mtu na mtu hutokea katika jamii). Angalia sasa anavyojichanganya, amesema hakuna kanuni inayotoa maelekezo ya kushughukia tatizo kama hilo hapo hapo anasema akirudia atashughulikiwa. Kwa kanuni zipi?? hapo anajua yeye.
 
Nafikiri naibu spika amegundua hawa watu wana uhusiano wa karibu sana hivyo ameamua bunge lisiingilie masuala nyeti ya watu binafsi.
 
Vazi livaliwe na wanaohusika kulivaa sio kuvaavaa tu. Kwan vazi hilo sio jezi mbeya city ila ni vazi maalum kwa wafuasi wa dini ya kiislam.
Kanzu ni vazi kama mavazi mengine, a halina mfungamano wowote na dini...ni kwamba tu wengi wa walio Waisilamu wamechagua kutumia vazi hilo...

Kwa wenye imani wengine ni viongozi wao ndio wamechagua kuvaa Kanzu ie Mapadre, Wachungaji n.k....na Waumini wao hubaki kuvaa tu nguo za kawaida.
 
Sis watanzania hatuna akili kabisa, hiyo nayo ni issue ya kudiscuss kweli? huwez kumvua kofia mtu usiyemfahamu, hawa watakuwa walikuwa na utani flani. Kuna haja ya kureview hiz Phd za watanzania, manake karibu wote ni zero kabisa.
 
Mwongozo wa kofia ni wa maana sana kwa huyo bi mdogo lakini si la watoto wa UDOM! Hopeless! Hatakumbukwa hata na mambulula wenzake ndani ya chama! Yeye ni tv tu kuubwa remote iko magogoni!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom