Naibu Speaker afuta kipengele cha Rushwa Mahakamani katika Hotuba ya Upinzani akidai hakina Ushahidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Speaker afuta kipengele cha Rushwa Mahakamani katika Hotuba ya Upinzani akidai hakina Ushahidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Said Bagaile, Jul 29, 2011.

 1. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [h=2]Jaji Kiongozi akemea rushwa mahakamani[/h]Wednesday, 24 February 2010 08:17 newsroom
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  NA FURAHA OMARY
  JAJI Kiongozi Fakihi Jundu, amewaasa watumishi wa mahakama, kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa miongoni mwao. Pia, amewataka mahakimu na majaji kuhakikisha wanatoa masharti ya
  dhamana yanayotekelezeka kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka kutoa adhabu mbadala ya kifungo ili kupunguza msongamano wa mahabusu na wafungwa magerezani, kwani hali inatisha. Alitoa rai hiyo jana mjini Dar es Salaam, alipofanya ziara katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuzungumza na mahakimu na watumishi wa mahakama hiyo na Wilaya ya Ilala. “Tunalalamikiwa kwamba tunapokea hongo, rushwa na mishiko. Sisemi wote wapo hivyo ila mahakimu na watumishi mwenye matatizo hayo wajirekebishe. “Wiki iliyopita nilitembelea magereza nimekuta wenzetu wapo kule, tuliyopo huku tujiepushe na mambo hayo,” Jaji Kiongozi aliwaasa watumishi hao. Alisema kuwa watumishi hao wanapaswa kujiepusha na tatizo hilo la rushwa, kwani anaamini inawezekana. Kuhusiana na hali magerezani, Jaji Kiongozi Jundu alisema inatisha, kwani kuna msongamano mkubwa, hivyo mahakimu na majaji ni wadau muhimu wa kuhakikisha hali hiyo inapungua au inaongezeka. Alisema magereza yamejaa, hivyo watumishi hao wanapaswa kuhakikisha kama sheria haiwabani, kutoa masharti ya dhamana kwa washitakiwa yanayotekelezeka na kuangalia adhabu wanazozitoa mbadala wa kifungo. Mbali na hilo, Jaji Jundu aliwataka mahakimu na majaji kutumia lugha inayofaa kwa watu wanaofika mbele yao kudai haki, ili kuwafanya wawe na imani nao wakati wakiendesha mashauri yao. “Kuna baadhi yetu utakuta watu wanakuja mbele yao, lugha wanayoitumia inamfanya mtafuta haki kukata tamaa kwa kutoa lugha inayoegemea upande mmoja. “Malalamiko hayo nayapata ya waheshimiwa kuonekana kuegemea upande mmoja, wote tuna udhaifu vizuri tulinganishe lugha ili watu wawe na imani,” alisema. Aidha, aliwasihi mahakimu wajipange vizuri mashauri wayasikilize kwa wakati na kumalizika kwa wakati ili kuondoa malalamiko ya kucheleweshwa kwa mashauri. Jaji Jundu alisema kuwa suala la kuahirisha kesi mara kwa mara bila ya sababu ya msingi halifai.

  Source Uhuru 24/2/2010
   
 2. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Jaji Mkuu akemea rushwa idara ya Mahakama [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 19 December 2010 20:18 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Tausi Ally
  WATUMISHI wa mahakama wametakiwa kuacha kupokea rushwa na badala yake wazingatie kanuni na maadili ya kazi.

  Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Mahakama ya Mwanzo Msoga/Lugoba mkoani Pwani,Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhan aliwataka watendaji wa mahakama kuacha tabia ya kuchelewesha kesi kwa makusudi kwa lengo la kushawishi rushwa.

  "Kitu kidogo iwe mwiko mahakamani, Mahakama imeweka sera ya kujenga majengo yenye kukidhi mahitaji yote yanayoambatana na shughuli za kutoa haki, hivyo hakuna sababu za kuchelewesha kesi,"alionya Jaji Ramadhan katika ufunguzi wa mahakama hiyo, iliyogharimu Sh 495 milioni.

  Jaji Ramadhan alisema mahakama hiyo ya Mwanzo ni mfano na inayoonyesha dira ya namna mahakama zinavyopaswa kuwa siku za usoni.

  Alisema mahakama ya Mwanzo Msoga ilianza mwaka 1935 chini ya mfumo wa kikoloni zikiitwa Local courts. Hakimu wake wa kwanza ambaye alikuwa anaitwa wakili ni Mzee Mrisho Kikwete ambaye ni babu wa Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Wakili Mrisho alijenga jengo dogo kwa mawe na kuezeka kwa nyasi na ndilo lililokuwa likitumika kama Mahakama wakati huo.

  "Ujenzi wa mahakama hii pamoja na kwamba ni moja ya mikakati ya kuboresha miundo mbinu, inalenga kutunza historia ya kutoa haki katika eneo hili,"alisema Jaji Ramadhan.

  Alisema mahakama ya Tanzania kwa kutambua hali ya miundo mbinu, imeweka sera ya kujenga majengo yenye hadhi ili kukidhi mahitaji yanayoambatana na shughuli za kutoa haki katika Mahakama.

  "Kwa msingi huo, ni sera ya mahakama ya Tanzania na majengo na nyumba ya Hakimu ya kisasa ili kuendana na sera yake ya kuajiri na kuwapanga mahakimu waliohitimu shahada ya kwanza ya sheria, katika vituo vya Mahakama ya Mwanzo,"alisema.

  Alisema majengo ya aina hiyo, yatawezesha utekelezaji wa sera ya mahakama ya Tanzania ya kuwa na miundo mbinu na vitendea kazi vya kisasa vitakavyoharakisha kutoa haki kwa wakati.

  Miundo mbinu hiyo ni pamoja na Kompyuta na mitambo ya kurekodi mwenendo wa mashauri mahakamani, ambayo tayari imeanza kutumika Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu Dar es Salaam, Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara na Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Anaesema hakuna ushahid anamaana gani????mbona hata MKULU ANALIJUA HILO,,,,,,,MIM NINAO USHAHID,NILIOMBWA HELA YA JUIS NA KARAN WA MAHAKAMA
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hivi hayo maelezo na habari ulizoweka juu unafikiri utakuwa ni ushahidi wa kuweza kutoa tuhuma?

  Kijumla kwa mwana taaluma yoyote ya sheria na mwenye akili timamu anaona wazi huo sio ushahidi kabisa wa kutoa tuhuma nzito kama hizo bali tunaita ni angalizo kwa wale wenye tarbia kama hiyo.

  namuunga mkono naibu Spika kwani siku zote Bungeni sio pahala pa kuzungumza umbeya au uzandiki ni pahala pa kutoa hoja zenye ueleo mkubwa na ushahidi tosha pasi na shaka.

  Pole sana.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kama wewe ni mkweli na unachukia rushwa, kwanini usipeleke kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake. Nafikiri kuna namna hapa.
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  i think RED ni JULY 2011
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba chombo chenyewe cha kupambana na rushwa hakiaminiki hata kama ukikiamini kiasi gani.

  Unawapigia simu ama unakwenda ofisini kuwaona kwamba kuna mtu kaniomba rushwa, kabla hawajaenda kumkamata wanampigia simu anajiandaa kukwepa mtego ama wewe ndo unageuziwa kibao kwamba ulitaka kutoa rushwa. Katika hali kama hiyo njia pekee inayobaki ni kuwatumia wabunge wafikishe kilio cha wananchi kunako husika.
   
Loading...