Naibu Mwanasheria Mkuu wa SMT na Waziri Ghasia Live Channel Ten Kuhusu Muswada wa Katiba

waende zao uko cha msingi hapa ni sisi kumshukuru Mungu kwa jinsi anavyoleta ukombozi kwetu kwa njia anazo zijua yeye na watazidi kuangamia kila mahali wataonekana wabaya kwa sababu habar yao kwisha sasa
 
Kimbunga,

Kwa miaka mingi Wanzazibari wamekuwa na malalamiko mengi na hata wengi wao wamekuwa wanatafuta namna ya 'kuutapika' huu muungano maana wanaona una-wadhuru! Ni vizuri kutambua kuwa takribani 80% ya wanzibari walizaliwa baada ya muungano na kama ilivyo Bara, visiwani nako hakuna mtu amekuwa anaeleza in details kwa nini hizi nchi mbili ziliungana zaidi ya kusema 'sisi ni ndugu wa-moja'! Hata hivyo muungano umekuwa 'unavumiliwa' zaidi na wana-ccm kuliko CUF. Na kama tujuavyo CCM inakubalika zaidi Unguja wakati CUF wao wameteka Pemba (100% - majimbo).

Sasa, kasheshe ni hivi; Wapemba ni wengi zaidi ya wa-Unguja na kwa mtaji huo Muungano unavumiliwa na watu wachache zaidi. Drama inazi pale CCM nao wanaanza kuukinai Muungano kama tulivyoshughudia wakati wa maoni ya muswada. Kauli za kejeli zinazotolewa na viongozi wa ccm including viongozi wa ccm wanzibari walio ndani ya Serikali ya muungano zinazidisha hasira kwa umma. Sijui ni kwanini mtu kama Samia Suluhu ambaye hata yeye mwenyewe aliwahi kuonesha kukwamishwa katika utendaji wa mipango ya SMZ wakati akiwa waziri Zanzibar analeta lafudhi za ccm-Tanganyika Zanzibar! hii ni inafanya watu wazidi kupaza sauti za kuutaka muungano uvunjwe. Nadhani mpaka hapo nitakuwa nimekudokezea something.
 
Hawa jamaa waoga kama makunguru. Wakati wananchi wanajadili mswada hata mmoja hakujitokeza kujibu hoja. Sasa wanaanzisha vipindi maalum kulaghai umma. Wanapoteza pesa na muda bure na wanazidisha hasira bora wangepotezea
 
Kuna Mheshimiwa mmoja wa CCM alinukuliwa na vyombo vya habari juzi baada ya kibano cha Mh Tundu Lissu bungeni akisema kuwa wao wana wanasheria waliobebea zaidi (kuliko Lissu I think). Niseme tu sikutegemea kama alikuwa anamaanisha Mh. Hawa Ghasia. Hivi huyu Mh. Ghasia si ndio yule Wizara imekuwa inalipa mishahara maruhani?!!! Huu utalaamu wa kuchambua kitu technical kama muswada wa katiba ya Jamhuri ya muungano katoa wapi wakati anashindwa hata kugundua maruhani (watumishi hewa) na kwenye orodha ya watumishi wa umma!

Kwa upande mwingine naona huu ni mwendelezo wa maadharau ya CCM kwa watanzania wa kutumia watao hoja hafifu na hata propaganda kwa mambo nyeti kama mjadala wa katiba. Kitambo kidogo walikuwa wanamtumia Tambwe Hiza sasa wanaona Hawa Ghasia is the right match? fedheha!
 
Mwanasheria anasema watoto wanahaki ya kujadili mswada. Na Zanzibar kuchoma mswada haisaidii chochote

kama katiba yenyewe imeweka kikomo cha umri wa m2 kuchagua kiongozi anaye mtaka. Namaanisha ni kuanzia miaka 18 (adult person). Huyo mtoto anayedai kuwa nayeye anahaki ya kuchangia katiba anamaanisha wa kuanzia umri gani, au hata wa kwangu aliyezaliwa mwaka jana naye 2mpeleke akachangie katiba. Pumba 2pu hapo, 2takua 2napoteza muda na malengo kutofikiwa. Wawe wanafikiria kabla hawajatamka.
 
BAhati mbaya sana kwa CCM na serikali yake ni kwamba hivi sasa waTanzania wengi hawaiamini tena hii serikali. Na imani hiyo imezidi kupotea baada ya kuamua kuurudisha serikalini huo muswada wa mabadiliko ya katiba. Hoja yoyote inayotolewa na serikali hivi sasa haiaminiwi tena na wananchi. Hivyo huyu mama wa Ghasia anapiga tu porojo.
 
Sijawahi kuona katuni kama "Ghasia'' maana huwa ni burudani kwa "watoto"
 
Back
Top Bottom