beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amewataka wagombea wa vyama vya siasa kuhakikisha kampeni zao hazivunji sheria kwa kusema uongo dhidi ya chama au mgombea mwingine.
Nyahoza aliyasema hayo jana katika mahojiano na chombo kimoja cha habari na kueleza kuwa matumizi ya uongo yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa chama kinachoongelewa vibaya.
“Kunapotokea uchochezi au matumizi ya maneno ya uongo au matusi, Msajili wa Vyama huchukua jukumu la kukemea vitendo vya aina hii pale wanapokuwa na uhakika wa kutendeka kwa vitendo hivyo,” alisema.
Pia alisema Msajili ana jukumu la kutoa onyo na adhabu kwa chama au mgombea endapo kutakuwa na ukiukaji wa aina yoyote wa sheria.
“Kwa kutenda kosa hilo pia kuna ulipaji wa faini kati ya Sh. milioni 10 na Sh. Milioni 50 na kukisimamisha chama kufanya shughuli za siasa kwa muda uliopangwa. Endapo mgombea atashinda uchaguzi ikiwa bado amesimamishwa atalazimika kusubiri muda ufike ndipo aendelee na majukumu yake ya kiofisi,” alisema.
Pia Nyahoza aliwakumbusha wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu kwa kuzingatia sheria za vyama vya siasa na kufuata taratibu za usajili ili kulinda kanuni zote za uchaguzi.
Chanzo: IPP MEDIA