Konakali
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 1,533
- 263
NAIBU Meya wa Jiji la Arusha ambaye ni Diwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), amewataka viongozi wa juu wa chama hicho kuacha kuwadanganya wakazi wa Jiji la Arusha kwamba watafanikiwa kumwondoa Meya wa Jiji hilo.
Diwani huyo wa Kata ya Kimandolu, Estomii Mallah, amemtaka Katibu Mkuu wa Chadema,
Dk. Willibrod Slaa na wenzake, kuacha kuwadanganya wananchi wa Arusha na Watanzania kuhusu sakata la umeya wa Arusha kwa kuwa hakuna tena njia ya kumtengua katika nafasi hiyo meya wa CCM aliyepo madarakani, Gaudance Lyimo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mallah alisema mbali na siku 30 za kisheria za kufungua shauri mahakamani la kumpinga meya huyo kupita, pia Dk. Slaa alikuwa na taarifa kuhusu muafaka uliofikiwa kati ya madiwani wa Chadema na CCM na aliubariki.
Hivi jamani kuna njia gani tena ya kumuondoa Gaudance pale na kusema hakuchaguliwa kihalali maana siku 30 za kisheria zimemalizika baada ya wao wenyewe viongozi kuvutana vutana na ahadi zao hewa sasa leo unawadanganywa wananchi kuwa hamuungi mkono meya mpaka lini, alisema Mallah.
Alisema amekuwa akipokea ujumbe mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Jimbo la Arusha
kuhusu ushauri wa yeye kuufuata, lakini alitumia njia hiyo kuwaomba radhi kuwa hatoweza kufuata ushauri wao kwa kuwa kutairudisha Halmashauri katika mvutano.
Aidha, amewaonya vijana na wananchi mbalimbali wanaoshabikia jambo hilo kuwa pindi vurugu itakapotokea, hawatakuwa na mahali pa kukimbilia zaidi ya vijijini kwao walikotokea
kwa hofu ya kudhurika.
Pia aliwaonya wafanyabiashara wakubwa wanaoendelea kusaidia malumbano, akisema hayana faida kwao zaidi ya hasara ya kusababisha biashara za hoteli na utalii kushuka kutokana na wageni kuhofia hali ya usalama wao Arusha.
Alishauri wananchi wa Arusha kukaa na kutafakari wenyewe jinsi ya kuirejesha amani iliyopotea kwani haiwezekani kusubiri watu wa nje kuja kuwapatanisha na kuwarejeshea amani hiyo kwa kuwa wao hawaathiriki na lolote pindi amani hiyo inapokosekana.
Alisema yeye na madiwani wenzake wanne waliovuliwa uanachama Chadema, hawana
ugomvi na kiongozi ye yote wa Chadema na ndiyo maana pindi walipopatiwa taarifa ya kuvuliwa uanachama walikimbilia mahakamani ili kudai kurejeshewa uanachama wao.
Source: Habari Leo; by John Mhala, Arusha; Tarehe: 6th October 2011