Naibu Meya wa Jiji la Arusha awapa somo viongozi wa Chadema...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Meya wa Jiji la Arusha awapa somo viongozi wa Chadema...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Konakali, Oct 6, 2011.

 1. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  NAIBU Meya wa Jiji la Arusha ambaye ni Diwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
  (Chadema), amewataka viongozi wa juu wa chama hicho kuacha kuwadanganya wakazi wa Jiji la Arusha kwamba watafanikiwa kumwondoa Meya wa Jiji hilo.

  Diwani huyo wa Kata ya Kimandolu, Estomii Mallah, amemtaka Katibu Mkuu wa Chadema,
  Dk. Willibrod Slaa na wenzake, kuacha kuwadanganya wananchi wa Arusha na Watanzania kuhusu sakata la umeya wa Arusha kwa kuwa hakuna tena njia ya kumtengua katika nafasi hiyo meya wa CCM aliyepo madarakani, Gaudance Lyimo.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mallah alisema mbali na siku 30 za kisheria za kufungua shauri mahakamani la kumpinga meya huyo kupita, pia Dk. Slaa alikuwa na taarifa kuhusu muafaka uliofikiwa kati ya madiwani wa Chadema na CCM na aliubariki.

  “Hivi jamani kuna njia gani tena ya kumuondoa Gaudance pale na kusema hakuchaguliwa kihalali maana siku 30 za kisheria zimemalizika baada ya wao wenyewe viongozi kuvutana vutana na ahadi zao hewa sasa leo unawadanganywa wananchi kuwa hamuungi mkono meya mpaka lini,” alisema Mallah.

  Alisema amekuwa akipokea ujumbe mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Jimbo la Arusha
  kuhusu ushauri wa yeye kuufuata, lakini alitumia njia hiyo kuwaomba radhi kuwa hatoweza kufuata ushauri wao kwa kuwa kutairudisha Halmashauri katika mvutano.

  Aidha, amewaonya vijana na wananchi mbalimbali wanaoshabikia jambo hilo kuwa pindi vurugu itakapotokea, hawatakuwa na mahali pa kukimbilia zaidi ya vijijini kwao walikotokea
  kwa hofu ya kudhurika.

  Pia aliwaonya wafanyabiashara wakubwa wanaoendelea kusaidia malumbano, akisema hayana faida kwao zaidi ya hasara ya kusababisha biashara za hoteli na utalii kushuka kutokana na wageni kuhofia hali ya usalama wao Arusha.

  Alishauri wananchi wa Arusha kukaa na kutafakari wenyewe jinsi ya kuirejesha amani iliyopotea kwani haiwezekani kusubiri watu wa nje kuja kuwapatanisha na kuwarejeshea amani hiyo kwa kuwa wao hawaathiriki na lolote pindi amani hiyo inapokosekana.

  Alisema yeye na madiwani wenzake wanne waliovuliwa uanachama Chadema, hawana
  ugomvi na kiongozi ye yote wa Chadema na ndiyo maana pindi walipopatiwa taarifa ya kuvuliwa uanachama walikimbilia mahakamani ili kudai kurejeshewa uanachama wao.

  Source: Habari Leo; by John Mhala, Arusha; Tarehe: 6th October 2011
   
 2. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mjadala wa Arusha ulishafungwa na maamuzi makini na ya busara yalishafanywa na Viongozi hodari wa Chadema, sasa wewe kama unajipya kasimulie familia yako.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135


  Uchaguzi wa madiwani utafanyika lini baada ya CDM kuwatimua madiwani wake?
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jiji la Arusha halina naibu meya, sasa sijui huyu anayetajwa hapa gazeti la jamboleo wamemtoa wapi? Huu ni uandishi wa habari wa ajabu sana.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Huyo mwandishi nadhani hajui kinachoendelea hapa nchini! Mallah sio diwani tena! Kwahiyo anamtambulisha kimakosa.
  Na huyu mallah anatafuta pa kujishika maana anaanguka. Aman gani imetoweka Arusha? Watalii wamepungua kwa kiasi gani! Leo anasema hana ugomvi na viongozi wa cdm! Kwann aliwapeleka mahakamani?
  Huyu ni mnafiki mkubwa and he's the one behind kutimuliwa kwake na wenzake. Sasa anatapatapa na kujifanya kutoa ushauri. Kama alijua haiwezekani kumwondoa meya mbona aliingia muafaka kwa kuhongwa badala ya kutumia busara? Apeleke ujinga wake huko!
  Wakazi wa Arusha wameshaamua kutokumtambua wala kumpa ushirikiano huyo mmea hadi sheria itakapofuatwa. That is the end of the story!
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibarika Arusha!
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Well done kwa ufafanuzi kumbe hizi kelele za kina Slaa ni za mavuvuzela ambao wanaujua ukweli ila hawataki kuusema
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ndio maana magazeti yote makini hayakuandika utumbo huu.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Thinker msiwe sinkers tfadhali leteni mijadala yenye tija na si huu ujinga .Mwacheni huyu mpuuzi na wapuuzi wenzake wa magazeti wana hangaika tu .Kama hana ugomvi haya anayo sema si ugomvi ?Ana mchonganisha Slaa na wananchi siyo ?Atoe ushahidi kama anao juu ya madai yake .
   
 9. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg Mala Ninakuheshimu sana, ningefurahi kama kwa sasa ungeamua kukaa kimya kabisa ili usisababishe machungu mioyoni mwetu. Sisi tunajua mpango mzima wa kuleta machafuko na vurugu zisizoisha hadi kipindi cha GodBless Lema kiishe bila maendeleo hapa Arusha. Lakini tuwaambie CCm kuwa hilo halitupi shida na CCM hatuitaki kabisa hapa Arusha, JK aendelee kuhamisha mikutano yetu muhimu huko Dar hilo pia hatujali, ila haya yote yanamwisho na siku moja atajibu!!!!!!!!!!
  Serikali inauwezo wa kuleata muafaka wa kudumu lakini imebaki kufanya kuwa CDM ndiyo wenye matatizo huu ni uzushi mtupu.
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Demkrasia na ndani ya vyama vya upinzani ni ndogo kuliko ccm

  CCM ni chama pekee ambacho wanachama wake wana demokrasia.

  Vyama vingine fuata amri kutoka uchagani hutaki kaa kimya ..
   
 11. magnificent

  magnificent Senior Member

  #11
  Oct 6, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa usitadhi, nenda katoe tamko. nikawaida yenu
   
 12. m

  mpiganaji86 Senior Member

  #12
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naww topical hapo juu unafuata amri kutoka kwenye masaburi ya bibi yako mzaa babu yako
   
 13. Beso

  Beso JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  gazeti la jambaleo!!!
   
 14. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Sikapendi hako kagazeti kakina malinzi kwa kujikomba sikajisali kama nikagazeti ka ccm??kagazeti uchwara kanatoa habari uchwara kwakufaata siasa uchwara!!
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kama kwa kutamka kuwa huyu msaliti ni diwani, pengine ni kwa sababu akili zake zishahama huyo. Angoje tu kugombea tena kupitia chama kingine
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  mkuu badili jina.maana unaonekana bongo yako imelala kabisa.
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Hilo gazeti siwezi kulisoma hata kwa kuchinjwa kwa msumeno
   
 18. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #18
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280
  huyu bado ni diwani?
   
 19. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  hakuna ulevi mbaya kama udini.maana upumbaza,upofusha na mwisho ni kujitoa mhanga!
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Mtaji wa wasioweza kutenda ni fujo.
   
Loading...