Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,410
- 8,807
Naibu meya wa Ilala Mh. Omary Salum Kumbilamoto, ametoa msaada wa vifaa kwenye zahanati ya Vingunguti. Vifaa hivyo ni :
1. Mizani ya kupimia uzito watoto;
2. Seti moja ya Television; na
3. Feni mbili
Aidha, Mh naibu-meya amehimiza na kutoa wito kwa viongozi wengine kuwa na utaratibu kama huo wa kutembelea katika maeneo yao ili kutatua changamoto zilizopo.
SOURCE: Habari za Saa - ITV.
My take;
Japokuwa mimi sio mwana-DarSlum, namtumia salaamu za 'bravoo' kutoka huku kwetu Nangurukuru. Binafsi nampongeza sana mkuu Kumbilamoto kwa moyo huo wa kiungwana na kiuongozi, na inshallah Mwenyezi Mungu ambariki zaidi.
Lakini sasa, kilichonishangaza mimi binafsi, ni kuona ''makamera'' na vyombo vya habari kwenye hiyo event! Je, kulikuwa na umuhimu au ulazima wa kuongozana na 'makamera' hapo zahanati ili kuifanya 'shuhuli' hiyo?
Ni jambo jema, lakini je hivi hawa viongozi wetu hawawezi kabisa kuwatumikia wananchi pasipo 'spotlight' ?!!
Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie mzigoni rasmi, hapa JF tumekuwa tukiwachana sana wale viongozi wote wenye mahaba ya makamera wanapokwenda 'site' kuwatumikia 'wadanganyika'. Sasa basi, ili kuondoa double-standard kwenye hii hulka ya viongozi wetu, 'makamanda' wote tuungane pamoja 'kumchana' na kumpa makavu live huyu naibu meya wa LA FAMILIA na viongozi wengine wote wenye 'mahaba-niue' with spotlight unnecessarily !
Ifikie mahala sasa viongozi wetu watambue kuwa wana wajibu wa kuongoza na kuzitumikia jamii zao bila hata makamera kwenye field. Kama wakizingatia UONGOZI SAFI, surely wataendelea tu ku-maintain their political mileage even without limelight!
-Kaveli-