Naibu meya CHADEMA nimejiandaa kukaa gerezani Kisongo

kuchangumu

JF-Expert Member
Apr 2, 2014
724
290
Naibu Meya wa Jiji la Arusha Prosper Msofe na Diwani wa Levelos, Ephata Nanyaro wote wa CHADEMA, wamesema wamejiandaa kukaa Mahabusu Gerezani Kisongo, ikiwa ni Ishara ya kupinga unyanyasaji na ubambikaji kesi unaofanywa na Jeshi la Polisi kutokana na mashinikizo ya Kisiasa. Ephata Nanyaro alisema, wakishafikishwa Mahakamani leo na kusomewa mashitaka hayo waliyodai kuwa ni ya kubambikwa, hawatakubali Dhamana, ili waende mahabusu hadi Siku nyingine ya kesi, kuwafanya Watawala waache kuwatishia Watu magereza. Hapa Nanyaro anasema, "Sisi tulipigwa na Mgambo, walitufungia 'Depot' wakatuchangia, na Wananchi wetu ni mashahidi kwani walikuwa nje na wao ndio walituita tukawasaidie kuwanusuru wenzao walionyang'anywa Mali zao bila utaratibu. Hivyo Wananchi wetu wanaujua ukweli kuwa baada ya Sisi kuingia pale Mlango ulifungwa, na Mgambo walituchangia, tulipigwa sana, kama mimi nilichanika mdomo na tulienda kutibiwa Zahanati ya Ngarenaro na Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, licha ya Polisi kukataa kutupa PF3".
 
unabambikizwa wakati ni kweli mlimpiga yule mwanamgambo wa kike mpaka akalazwa, wewe usilete siasa hapa, hata sisi ndugu zake tunataka huyu dada apate haki yake, mmetupigia dada yetu alafu mnaleta siasa hapa, haki lazima tupate, tunasema tena haki ya dada yetu lazima ipatikani, ninarudia tena dada yetu lazima apate haki yake,
 
Mgambo wa jiji kufanya kazi kwa remote control - Poleni makamanda haya yote nayakaribia mwisho wake!!
 
unabambikizwa wakati ni kweli mlimpiga yule mwanamgambo ya wa kike mpaka akalazwa, wewe usilete siasa hapa, hata sisi ngugub zake huyu dada ambaye mimi ni mama yangu mdogo hatutakubali, mmetupigia dada yetu alafu mnaleta siasa hapa, haki lazima tupate, tunasema tena haki ya dada yetu lazima ipatikani, ninarudia tena dada yetu lazima apate haki yake,

nipe jina la mama yako mdogo
 
hakuna kesi hapo, mwisho wa siku hushahidi hautapatikana.hao mgambo wana kiherehere sana wana takiwa walipishwe vitu vya watu walivyochukuwa na kugawana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom