Naibu katibu mtendaji baraza la mitihani aondolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu katibu mtendaji baraza la mitihani aondolewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CHANGA, May 29, 2009.

 1. C

  CHANGA Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Aliyekuwa Naibu katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani ameondolewa kwa kuhamishiwa Taasisi ya Elimu kuwa Desk Officer. Sababu hazijaelezwa zaidi ya kuitwa kuwa ni uhamisho wa kawaida. Anayechukua nafasi yake ni Mtu anayeitwa Tamamu aliwahi kuwa mkaguzi wa shule Kanda ya Kaskazini Mashariki, Kilimanjaro. Sijui kama ni mbinu za kuondoa uozo wa Baraza hilo au ni Tabia ya Ndalichako kuwaondoa wale wanaotofautiana na utawala wake. Mwaka 2006 ndalichako huyo huyo alimwondoa Naibu wake bwana Mbiku na Kumhamisha Ilboru Sec na baadae mwaka huo huo kuwaondoa Maafisa Mitihani 31 waliopelekwa shuleni kufundisha. Sijui mbinu hii ni ya kusaidia kuliweka baraza hilo kuaminika katika jamii au ni kuliangamiza kabisa. nawsilisha
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Alhudaism......!
   
 3. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #3
  Jun 1, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kifupi huyo mama kazi imemshinda kuna watu wengi tu hapo wanaliharibu baraza la mitihani e.g Mafie lakini anawakumbatia
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  hamjui kuwa nae ni nyoka....??ukiwa nyoka unalindwa hata ukiharibu...mmesahau yule mama wa NIC???na wengine wengi tuu??
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa, hivi Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani ana uhusiano gani na uhamisho wa Bw. Mbiku kwenda kufundisha Ilboru? Naamini kuwa uwezo wa kumhamisha mfanyakazi kutoka Baraza kwenda kufundisha uko chini ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu au/ na Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari katika Wizara ya Elimu na si Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani.

  Katibu Mtendaji wa Baraza ana uwezo wa kum-demote mtu na kumpangia kazi nyingine ndani ya Baraza la Mitihani (ndani ya utawala wake) na si nje ya hapo.
   
 6. Sabode

  Sabode Senior Member

  #6
  Jun 1, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hii Kazi kweli kweli.
  Nasikia pia watoto wa form six ambao walikuwa hawaja kamilisha credit na waka reseat wakiwa form five wanatakiwa kufanya paper kama PC vinginevyo wafanye mtihani 2011!!! wana Jamvi mlo jikoni hube naomba mnipakulie ukweli wa hili.
  Heshima mbele
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kazi kubwa kwa sasa ni kulisafisha Baraza la Taifa la Mitihani. Ieleweke kuwa kila CEO ana uwezo wa kufanya mabadiliko ndani ya eneo lake la kazi. CEO anaweza tu kuhusika katika uhamisho wa nje kama atatoa maoni kwa mwajiri wake kuhusu kutoridhika kwake na utendaji wa mfanyakazi katika utawala wake na anaomba ahamishwe. Tukumbuke kuwa Intelligence iko pale NECTA kuchunguza maovu ya pale, hivyo uhamisho kwa sasa is inevitable kwa baadhi ya vingunge, na wengine hawatakuwa desk officers tu bali watafukuzwa kazi kabisa. Taratibu itakuwa kuwahamisha na kuwafanya officers/or kupewa kazi yoyote ile pindi upelelezi kamili utakapotimia na evidence ndipo vibarua vitaota majani. Hata Bi Ndalichako naye yuko ndani ya upelelezi, hivyo si kwamba yeye amepona bali itafahamika kama anahusika na uovu wowote pindi kazi ya UWT itakapokamilika.

  Tungependa, tuwe na wasomi wa kiuhakika si wa siku hizi wa vyeti vya kununua madukani. Enzi zetu kama mtu ulipata div one yaani ni mkali na unakuwa unategemewa, eti siku hizi hata kifuniko wa darasa anapata div one halafu yule mtoto wa maskini ambaye hawezi kununua mtihani anapata say div 2 or one ya struggle. Huku maofisini maofisa tunawaambia andika report ni tabu tupu, bosi unakuwa unafanya editing mpaka mwishowe unaamua kuandika peke yako. Tumechoka.
   
 8. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kiuongozi ,huyo kiongozi wa Baraza, anaUWEZO wa KUMSHAURI Katibu Mkuu Wizarani kuhusu mtumishi yeyote aliyepo chini yake.Katibu mkuu normally ANABARIKI ushauri aliopewa.

  Hivyo uwezo unaozungumzwa hapa wa huyo mama ni katika "mazingira" hayo.
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo taasisi nyingi za Serikali zinaendeshwa Kisiasa na si kitaaluma,inafutwa sera ya CEO si ya Taasisi.
   
 10. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2009
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Mabadiliko ni lazima, hakuna aliyeumbwa/zaliwa ili akae na kuongoza sehemu moja tu. Na mtu anapofanya vizuri anapongezwa na kupandishwa cheo, na anyeharibu anatakiwa kushushwa au kufukuzwa kazi kabisa iliwengine wenye uwezo zaidi yake wafanye kazi. Kwahiyo kuhamishwa kuwa Desk officer, inaweza kuwa ni njia ya kusafisha lakini bado iwe hatua ya kujenga na si kutengeneza tu mianya ya wajanja wengine.
  Uzi ungekuwa imara nina imani hata idara na taasisi nyingine zingefanya hivyo bila kukumbatia vihiyo kwa kujuana na vimemo!!!!
   
 11. Sabode

  Sabode Senior Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Habari tena Jamvini.
  Kuhusu swali langu hapo namba sita kuna mwenye habari naomba kufahamu wazee.
   
 12. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama hawajamaliza unategemea nini Mkuu, mimi naona ipo poa sana tuuuu.
   
 13. Sabode

  Sabode Senior Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kunta naona hujanielewa
  Nazungumzia walio maliza na wamekamilisha kabisa naomba nifahamu hili sio wale ambao hawajamaliza umenisoma mzee?

  Jambo jingine kuna namna ya kusoma matokeo ya form IV 2007 naona kwenye mtandao wa necta hayapo ina maana wemesha yaondoa? au hawa sever kubwa za kutosha?
   
Loading...