Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi aongoza kikao cha Makamishna wote wa Jeshi la Uhifadhi Tanzania

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akisisitiza kuhusu umuhimu wa kupitia vema Miundo ya Taasisi za Uhifadhi ili kuliwezesha jeshi hilo kutenda kazi zake kiutaalam zaidi na kwa ufanisi mkubwa huku Taasisi za Uhifadhi zikizingatia kuimarisha Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu na kudhibiti ujangili.

kikao hicho cha kujadili na kupitia Miundo ya Taasisi ( Organization Structure) ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, kimehudhuriwa na Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi za Uhifadhi za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
1597751888162.png

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akifuatilia kwa umakini michango ya wajumbe wakati wa kikao chake na Makamishna wa Uhifadhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki

1597751944564.png

Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Fredy Manongi, akisisitiza kuhusu utekelezaji wa sheria kwa watumishi wa Jeshi la Uhifadhi ili kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya katika nyanja zote.

1597752010189.png

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha ( aliyevaa uniform za JWTZ , kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi - Usimamizi wa Sheria na Mikakati ya Ulinzi na Usalama, John Nyamhanga ( kulia) wakifurahia jambo kufuatia michango ya wajumbe wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
 
Kuna watu wanawadalalia misitu ya vijiji na kupiga pesa ndefu hiyo nayo ni aina mpya ya UJANGILI
 
Back
Top Bottom