Naibu Katibu Mkuu wa UV-CCM Asimamishwa!

Nadhani Laana ya Nape imeanza kuisafisha UV-CCM. Inafuata miaka 5 ya majuto kwa UV-CCM kuziacha mbivu na kukumbatia mbichi kwa matumaini ya kuzivundika mpaka ziive, kumbe ni mbichi changa, hivyo lazima zitavunda na 'La kuvunda...
 
Ninachojua hiyo ni Kamati ya Utekelezaji wala haina uwezo wa kumfuta kazi Francis. Wenye uwezo na mamlaka ya kikatiba ni Kamati Kuu ya CCM. Kwa hiyo FMES umetuletea umbeya na maneno ya kijiweni. CCM oyee
 
Kwa hiyo aliyeleta hii breaking news ni muongo, bwa! ha! ha! ha! ha! hah!

Hapana Mheshmiwa Uwiano maalum,

Siwezi kumuita mleta habari muongo. Nadhani tu chanzo chake sio cha uhakika au chanzo chake cha habari kiliteleza. Kuna mushkeli kweli lakini sio kusimamishwa. Hayo ya kusimamishwa yanaweza kufuatia baadaye na vikao husika.

Ni tofauti ndogo tuu.
 
Unajua hizi habari huwa zinakuwa na source. Member wa JF wapo all over the world (nazungumzia Watanzania). Hawa members nao hupata taarifa kwa source zao wanazozifahamu na pengine kuziamini. Hivyo, kumshambulia member anapo post issues si halali sana. Japo kweli nafahamu kuna wazushi tu ambao wanataka kuleta hoja fulani pengin kwa lengo la ku mislead watu hasa wanapokuwa wana issues muhimu ya kuchangia kama ilivyo ya Anne Kilango na Matayo huko Same.

Kwa sababu hiyo basi pengine aliyeleta hii issue akaidakiza kwa FM ES ni ili misdirect attention yake kwa issue ya Anne. Vinginevyo, wote tusubiri tuone kama kweli huyo jamaa hajasimamishwa uongozi au la since it is still Breaking News.

Leteni habari kwa wale ambao wameshapata uhakika kama jamaa katimuliwa au ni uzushi.
Wajameni hii 2009 hadi dead days za uchaguzi 2010 tutaona mambo.

Mafisadi wasituue tu ili tuishi tuuone mwaka 2010. Print and electronic media zitaongezeka, wazushi, mamluki, vibaraka,, waongo, wambea, wapambe, du you name all.
 
Hapan uwiano maalum,

Siwezi kumuita mleta habari muongo. Nadhani tu chanzo chake sio cha uhakika au chanzo chake cha habari kiliteleza. Kuna mushkeli kweli lakini sio kusimamishwa. Hayo ya kusimamishwa yanaweza kufuatia baadaye na vikao husika.

Ni tofauti ndogo tuu.
JF siku zoote tunataka habari zenye uhakika.....watetea taifa na sio walevi wanakuja na news za uhakika.....kasema
wa tuhuma za ubadhirifu wa pesa, amesimamishwa kuanzia leo tarehe 18. 2. 09.
kama chanzo hakiamini angatafiti kwanza kabla ya kurukia na kujaza space jf kwa habari isiyokuwa na uhakika....
 
- Habari nilizozipata sasa hivi toka ndani ya CCM, zinasema kwamba Naibu katibu wa UV-CCM ndugu Francis Isaack, amesimamishwa kazi hiyo mara moja kwa tuhuma za ubadhirifu wa pesa, amesimamishwa kuanzia leo tarehe 18. 2. 09.

Tutakuwa na habari zaidi as soon zitakapopatikana..!

Hichi ndicho kichekesho cha CCM. Huyu katafuna mabilioni mangapi mpaka kasimamishwa? Hawa akina Lowassa, Msabaha, Chenge, Mramba, Mgonja, Karamagi, Rostam Azizi mbona bado wanapeta tu ndani ya chama!? Lini watasimamishwa ubunge (kwa wale ambao ni wabunge) kutokana na ufisadi walioufanya dhidi ya Watanzania? Huu ni unafiki mwingine wa CCM.
 
Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba Bw Francis Isaac ni mmoja wa vijana waliomwakia sana Nape wakati alipofichua masuala ya ufisadi katika uuzaji wa jengo la UVCCM pale Lumumba, kwa hiyo napa picha ya alichokuwa akikitetea.
Hata kama habari hizi za kusimamishwa kwake hazijathibitishwa, lakini bado Isaac si msafi kabisa.
 
- Habari nilizozipata sasa hivi toka ndani ya CCM, zinasema kwamba Naibu katibu wa UV-CCM ndugu Francis Isaack, amesimamishwa kazi hiyo mara moja kwa tuhuma za ubadhirifu wa pesa, amesimamishwa kuanzia leo tarehe 18. 2. 09.

Tutakuwa na habari zaidi as soon zitakapopatikana..!

Kamanda

Tunakuomba uje uthibitishe hizi news maana nijuavyo April 1 bado iko mbali.

Asante
 
- Habari zaidi ni kwamba Bwana Francis jana aliitwa na kikao maalum cha kamati ya utekelezaji na kutakiwa kujibu tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake, hasa katika sihu ya ukarabati wa ofisi ya jengo la Vijana makao mkuu.

- Tuhuma ya kwanza ni kwamba amekua akiwapatia tenda Wahindi kwa siri kufanya ukarabati wa jengo, kwa vipande vidogo vidogo na hata kuwaruhusu baadhi yao kugeuza vipande hivyo apartments zao.

- Tuhuma nyingine ni kuwa ameiba hela za umoja huo zipatazo shillingi millioni 16, huku akionyesha risiti za halali za shillingi millioni sita tu!

- Mbele ya kikao hicho jana, alikiri baadhi ya makosa yake, huku akikana mengine, kamati iliamua kumfukuza kabisa umoja huo, lakini the dataz ni kwamba kuna wakubwa wa taifa walioingilia na kudai asimamishwe tu kwanza for now, kikao hicho kilimchagua mwanachama wake wa siku nyingi Bwana Ali Isa toka Pemba, aliyewahi pia kwua DC wa Chake, kuikaimu nafasi hiyo mpaka ufumbuzi utakapopatikana.

- Pia kikao hicho kilimchagua Ridhiwani, pamoja na Marwa Mtahayo na wengineo kama wanne kuunda kamati ya uchunguiz wa kina wa madhara yote yaliyofanywa na Bwana Isaack. Habari zaidi zinasema wkamba gazeti la Mwananchi limemhoji Bwana Isaack, aliyedai kwamba habari hizi sio za ukweli, lakini alipohojiwa Bwana Ali Isa amethibitisha kwamba ni kweli kuwa toka jana yeye ni kaimu mpya wa nafasi hiyo.

Sasa kuna habri kwamba mafisadi wamepania sana kuhakikisha kwamba habari hii haipewi au kupata nafasi kwenye media.

Kwa sasa ni hizo tu wakulu, later zikipatikan zingine!
 
pyepyere kibao.....unamwaga habari ambazo hazijathibiishwa hebu dhibitisha uzije na maandishi marefu kama hotuba za jakaya ndani hamna kitu....
Kidumu chama cha mapinduzi.

Francis hajasimamishwa wala kufukuzwa mpaka sasa hivi ninapoandika.

Habari ndio hiyo!
Usisingizie eti haipewi nafasi kwenye media ni kwamba hajafukuzwa period......wewe dishi lako lilinasa Sri lanka......
 
Kutoka Mwananchi ya Leo. FMES you are on top of the news, man!

Date::2/19/2009 Umoja wa Vijana CCM waanza kutimuana Na Leon Bahati
MGOGORO upya unafukuta ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapiduzi (UVCCM) baada ya Kaimu Katibu wake Mkuu, Isaack Francis, kuenguliwa kwenye madaraka kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali na matumizi mabya ya madaraka.

Baada ya kumtuimua Isaack, nafasi ya Kaimu Katibu wa UVCCM, inashikiliwa na Ally Issa, ili kupisha uchunguzi huru dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zimesema kuwa uamuzi wa kumwengua Katibu Mkuu huyo, umefikiwa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilichofanyika siku mbili kuanzia Jumanne chini ya Mwenyekiti wa umoja huo Masauni Hamad Masauni katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinasema kuwa, baada ya kumwengua Isaack, kamati imeunda tume ya watu watano inayoongozwa na Ridhiwan Kikwete kuchunguza tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa habari hizo, Isaak anatuhumiwa kuingia mkataba na wafanyabiashara wa jengo la Makao Makuu ya UVCCM bila kuijulisha Kamati ya Utekelezaji na Baraza Kuu la umoja huo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Kwa mujibu wa kanuni za UVCCM, kabla ya mikataba kutiwa saini, inatakiwa kupitia kwenye Kamati ya Utekelezaji, Baraza Kuu na Baraza la Wadhamini.

Taarifa za ndani ya kikao cha kamati ya utekelezaji zilieleza kuwa, baadhi ya wajumbe walikuja juu na kutaka Isaack afukuzwa kazi moja kwa moja kwa sababu maelezo juu ya tuhuma zake yako wazi.

Hata hivyo, Mwananchi lilipowasiliana na Issack, alikanusha taarifa hiyo akisema, tuhuma hizo sio za kweli na kusisitiza kuwa yeye bado yupo kwenye madaraka hayo ya Kaimu katibu Mkuu wa UVCCM.

"Hiyo siyo kweli. Mimi bado naendelea na kazi. Kwa sasa nimetoka tu kidogo ofisini niko maeneo ya Kariakoo," alisema Issack wakati akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu.

Hata hivyo alikiri juu ya kuandamwa na tuhuma hizo na kusema kuwa, waliozianzisha walikuwa na tafsiri tofauti.

Isaack alieleza kuwa katika shughuli za ukarabati wa jengo la UVCCM makao makuu, baadhi ya mafundi waliweka vifaa katika chumba kimoja cha jengo hilo na baadhi ya wanachama wakatafsiri kuwa wamepangishwa.

"Hii ni sehemu tu ya shughuli za ukarabati wa jengo na wala sikumpangisha mtu," alisema Isaack nakubainisha kuwa katika shughuli za ujenzi zinazofanyika katika eneo hilo, kuna wanaokarabati jengo na wanaojenga eneo la wazi nyuma yake.

Akizungumzia suala hilo, Ali Issa ambaye aliteuliwa kukaimu nafasi ya Isaack, alikiri kuwa tayari ameshaanza kazi hiyo.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Masauni Hamad Masauni hakupatikana ili kufafanua suala hilo jana baada ya simu yake ya mkononi kuita muda wote bila kupokelewa.

Mgogoro huo umekuja miezi michache tangu Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Nape Nnauye, kulituhumu Baraza la Wadhamini la UVCCM kuwa limesaini mkataba wa wawekezaji wa jengo hilo kinyume na taratibu.

Nape alidai kuwa baraza hilo na kumtaka mwenyekiti wake, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiuzulu, kwa madai kuwa mchakato wa ukarabati wa jengo hilo una harufu ya rushwa.

Tuhuma hizo zilikanushwa vikali na UVCCM na hata mkutano wa Baraza Kuu uliofanyika Dodoma Oktoba,mwaka jana kiliamua kumvua uanachama kwa madai ya kusema uongo.
 
- the more dataz ni kwamba rais jana aliwaagiza Umoja huo wa Vijana kwamba wampe wiki chache zijazo ili awapatie katibu mkuu mpya.

Tutaendelea kuleta more info as soon as tukizipata tu!
 
Kidumu chama cha mapinduzi.

Francis hajasimamishwa wala kufukuzwa mpaka sasa hivi ninapoandika.

Habari ndio hiyo!

Jasusi Re: Naibu Katibu Mkuu wa UV-CCM Asimamishwa!

Kutoka Mwananchi ya Leo. FMES you are on top of the news, man!

Date::2/19/2009 Umoja wa Vijana CCM waanza kutimuana Na Leon Bahati
MGOGORO upya unafukuta ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapiduzi (UVCCM) baada ya Kaimu Katibu wake Mkuu, Isaack Francis, kuenguliwa kwenye madaraka kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali na matumizi mabya ya madaraka.

Baada ya kumtuimua Isaack, nafasi ya Kaimu Katibu wa UVCCM, inashikiliwa na Ally Issa, ili kupisha uchunguzi huru dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zimesema kuwa uamuzi wa kumwengua Katibu Mkuu huyo, umefikiwa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilichofanyika siku mbili kuanzia Jumanne chini ya Mwenyekiti wa umoja huo Masauni Hamad Masauni katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Bwa! ha! ha! ah! ah! oooooooh! aibuuu mtumzima!
 
Hapana Mheshmiwa Uwiano maalum,

Siwezi kumuita mleta habari muongo. Nadhani tu chanzo chake sio cha uhakika au chanzo chake cha habari kiliteleza. Kuna mushkeli kweli lakini sio kusimamishwa. Hayo ya kusimamishwa yanaweza kufuatia baadaye na vikao husika.

Ni tofauti ndogo tuu.

- Mkuu FP, kweli hata wewe mtumzima ninakuheshimu na ninajua kwua una sources kibao hapa bongo, unaweza kukurupuka namna hii? Wewe kweli unaweza kushindana na dataz zangu mkuu unajua ninakozitoa?

- Sasa unaona aibu hii? Niambie tunaendaleaje mbele na mtu tuliyekua tukiheshimiana kama wewe after this? Maana hata ukiomba radhi haiwezi kusaidia what you did ni more than kukurupuka, halafu not from you mkuu? Kama Halisi hajasema kitu kuhusu uongo wa dataz zangu wewe kaaa pembeni mkuuu, maana ni yeye tu mut mmoja mwenye almost the same access kama zangu.

Hii ni aibu sana mkuu, hivi unajua kuwa huyu kijana kila akiulizwa kuhusu maadili amekua akijibu kwa kiburi kwamba aulizwe Nchimbi? Bwa! ha! ha! ha!
 
Back
Top Bottom