Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Naibu Katibu Mkuu wa CUF - Maalim, Nassoro Mazrui, akiongea na Mwananchi jana, alieleza imani yake kuwa, mgogoro wa Chama chao utamalizika na Maalim kuendelea kuwa Katibu Mkuu na kwamba suala la kuwania urais kupitia Chama kingine halipo. "Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif hawezi kukubali kuwania urais kupitia CHADEMA hata siku moja."
Mazrui aliongeza kuwa: Maalim hawezi kabisa kuhamia chama kingine kwa sababu ana wafuasi wake huku na wanaujua msimamo wake hivyo kinachotakiwa ni kuomba hatima ya mgogoro wa Chama ufikie mwisho tu lakini Maalim kuwania urais kupitia huko."
Aidha, msemaji wa Chama hicho, Mbarala Maharagande alisema kuwa, hilo la CHADEMA ni wazo zuri lakini uamuzi mgumu kama huo unatakiwa kutolewa na Vikao vya Baraza Kuu la CUF. "Ni kweli tumepokea ombi hilo ingawa sijajua wamekaa na Maalim wakaongea kuhusu hili. Muda ukifika Baraza litafanya uamuzi."
Mbarangande alimalizia kuwa: "Mgogoro wa Chama hicho utamalizika Oktoba."
Hata hivya, mnamo Mei 2017, Katibu Mkuu, Maalim Seif alikaririwa na Mwananchi akisema kuwa, hawezi kuhamia CHADEMA hata kama Chama hicho kitaendelea kuwa na mgogoro hadi wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao."